Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud akiwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon
Huwezi kusikiliza tena

Hassan Sheikh Mohamoud kwenda Daadab

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud hii leo anatarajiwa kutembelea kambi ya Daadab ambayo iko kaskazini mashariki mwa Kenya. Daadab ni miongoni mwa kambi za wakimbizi ambayo ina idadi kubwa ya wakimbizi walioishi kwa zaidi ya miaka ishirini na tano.

Hata hivyo, hivi karibuni, serikali ya Kenya imesema wakati umefika kwa kambi hiyo kufungwa. Awali mwandishi wa BBC Regina Mziwanda alizungumza na Bashkash Jugsoday ambaye yuko Garissa nchini Kenya na kumuuliza je Rais wa Somalia anaweza kuwa na ujumbe gani kwa wakimbizi na serikali ya kenya?