Mwili wa Muhammad Ali kuzikwa Ijumaa

Image caption Muhammad Ali

Mwili wa Muhammad Ali umewasili katika mji wake wa Louisville, Kentucky ambapo mazishi yake yatafanyika siku ya Ijumaa.Jeneza la nguli huyo wa masumbwi nchini Marekani ulisafirishwa katika msafara wa magari uliotokea katika uwanja wa ndege wa Louisville mpaka katikati ya mji.

Ali ni miongoni mwa wanamichezo mashuhuri waliofanya vizuri katika karne ya ishirini na salamu za rambi rambi zinaendelea kumiminika kutoka shehemu mbalimbali baada ya kifo chake kilichotokea siku ya Ijumaa.

Mazishi yake yanatarajiwa kuwa makubwa.