http://www.bbcswahili.com

04 Februari, 2009 - Imetolewa 14:45 GMT

Mpenzi wangu hataki kuvaa kondomu

Watu wengine hawapendi kutumia kondom, lakini ukweli ni kuwa – watu wakichagizwa kati ya kufanya mapenzi kwa kutumia kondom na kutofanya mapenzi kabisa, wengi huchagua kondom!

Basi tafakari - na ukichagua kutumia kondom jadili swala hili na mpenzi wako na muafikiane mapema, hata kabla hamjaanza kwani huenda kajisahau mkiwa katika lindi la nyege!

Halafu linabaki kuwa wazo tu kichwani je tutumie kondom, je ipo? na mambo kama hayo. Kama hamuwezi kujadili swala la kondom na yule unaemwita mpenzio, je huyo ni mpenzi wa kweli?

Kuwa mwazi - toa sababu zako za kutaka kutumia kondom, mfano wa sababu mwafaka nikama

Kama atakuwa bado hajashawishika kutumia kondom au hata anajaribu kukushawishi msiiitumie, ni haki yako kukataa kufanya mapenzi nae. Jiheshimu, na kama mpenzio hajali maoni yako basi mpenzi huyo hakufai, kwa hivyo hustahili kamwe kufanya mapenzi nae. Kumbuka hatua yoyote utakayochukua ni uamuzi wako. Sije ukajikuta unajuta baada ya kukubali matakwa ya mpenzio.

Wanaume wengine hutoa kila kisingizio na kisababu cha kutotaka kutumia kondom … Huenda akakwambia:

"Ninataka kuwa karibu nawe zaidi mpenzi! Nakupenda sana! kwani wewe hunipendi?" ...

"kufanya mapenzi na kondom ni kama kula peremende na karatasi yake!"...

"Kwa mara moja tu, basi tufanye leo kesho tutatafuta hizo kondom" ...na kadhalika

Hapo una mawili ya kuchagua.

1. Unaweza kuendelea kucheza mchezo wa mapenzi bila kuingiliana.

2. Unaweza kufunga virago na kujiendea zako!