Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 29 Januari, 2009 - Imetolewa 16:30 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Masimulizi ya washiriki
 
Kutokana na uhakika wa hadithi zenye uthabiti za wahusika wakuu wa kipindi chetu, wasikilizaji wameweza kwa urahisi kutambua, na kuhisi maono yao na hivyo kujifunza kutokana na simulizi ya maisha ya wahusika wakuu.

Huwa tunafanya utafiti na kuwachagua wahusika wakuu kwa misingi ya wao kuwa vijana wa kawaida wanaokabiliana na maswala ya kila aina ya afya ya uzazi.

Washiriki wa Kimasomaso huko Kisumu nchini Kenya.

Vijana hao kisha hurekodi hadithi zao angalau kila wiki ili kuelezea visa tofauti katika maisha yao na ambavyo wanakabiliana na maswala husika.

Baadhi ya Wahusika wakuu wa kipindi katika awamu ya pili walikuwa wafuatao.

Msichana Esther 'survivor'
• Esther (mwathirika wa ubakaji) Hii ni hadithi ya msichana aliye kuwa na umri wa miaka 18 alipobakwa katika party, baada ya kinywaji chake kutiwa dawa. Alipima na kupata hakupata virusi vya HIV lakini akashika mimba.

Hakuweza kujua ni vijana wangapi walimwingilia wakati huo alipokuwa bado bikira. Hakumueleza yeyote wakati huo, miezi michache baadaye akagundua kwamba alikuwa mja mzito.

• Allan (mzazi mwenye umri mdogo asiye na ajira).

• Prosper & girlfriend (wapenzi wanafunzi) – Ni hadithi ya wapenzi wachanga ambao wangali katika shule ya msingi katika kanda ya Buyenzi mjini Bujumbura, na ambao wanakumbana na maswala kama vile msukumo rika, elimu pamoja na maswala mengine ya afya ya uzazi ukizingatia kuwa wameshaanza kushiriki ngono.

Kijana Mukasa
• Mukasa (kijana aliye shoga) – Kijana huyu mwenye umri wa miaka 23 anaishi katika jamii yenye msimamo mkali dhidi ya ushoga huko nchini Uganda. Tunamulikia maswala ya ngono salama hasa miongoni mwa mashoga.

• Michael (kijana mdogo anaeishi na virusi vya ukimwi) – Kijana huyu alie-ambukizwa virusi akiwa na umri wa miaka 13 anahadithia jinsi anavyo-ishi kwa imani licha ya kuambukizwa kwa njia ya kusikitisha. Swala la umaskini pia linachipuza kwenye simulizi yake.

• Peris – Muelimishaji rika anayenakili vipindi vyake vyote na maisha yake kama muelimishaji rika.

Makala ilivyoendelea, watayarishi wa kipindi waliwapata wahusika wengine zaidi na kuwasiliana nao, aidha moja kwa moja au kupitia mtandao wa ripota wetu wa idhaa ya Kiswahili ya BBC katika eneo zima.

Kulikuwa na changamoto ya kuhakikisha kuwa wahusika na hadithi zimepatikana kutoka kwenye eneo lote linalofikiwa na idhaa ya BBC ikiwemo eneo la maziwa makuu na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Tanzania na Kenya.

Mbali na tatizo la kuendelea kuwasiliana na watu walioko kwenye eneo hili zima na ambao sio wataalam wa utangazaji, kipindi kilifaulu katika kuwahusisha vijana wa tabaka mbalimbali na maswala mengi kuhusu afya ya uzazi yanayowakumba vijana katika eneo la Afrika Mashariki.

Shindano la `Mfanyabishara Chipukizi Faidika na BBC`

Shindano la Mfanyabisahara Chipukizi Faidika na BBC Idhaa ya Kiswahili ya BBC London lililozinduliwa kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya idhaa hiyo linaingia mwaka wake wa tatu mwaka huu, 2009.

Kama alivyosema mkuu wa idhaa Solomon Mugera, shindano hili ni kwa ajili ya vijana wenye umri kati ya miaka 16 hadi 24 na kwamba washiriki wanapaswa kuandika mchakato wa aina ya biashara ambao utafafanua jinsi watakavyoiendesha kwa bajeti ya dola elfu tano za kimarekani wastani wa shilingi milioni tano za Tanzania.

Mshindi wa Faidika na BBC mwaka 2008, Ashura Kisesa.

Mwaka wa 2008 mshindi alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Burundi Ashura Kisesa ambae tayari ameshaanza mradi wake wa kuunda vyoo vya umma kwa malipo.

Watayarishi wa kipindi Kimasomaso Amina Abubakar na Tom Japanni wakiwa na Ashura Kisesa (katikati)

Hakika shindano hili mwaka limewavutia wasikilizaji wetu wengi sana, na hata katika fainali ya kwanza kabisa mwaka 2007, akitoa zawadi, mgeni rasmi katika hafla hiyo, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, mbali na kuipongeza BBC kwa shughuli pevu kama hiyo, aliomba shindano kama hili lirudiwe, na sisi bila hiana, tumefanya hivyo tangu hapo.

Kama ilivyokuwa mwaka jana, mwaka huu shindano hili litakuwa na awamu mbili:

Awamu ya kwanza: Kila nchi itakuwa na shindano lake, ambapo atapatikana mshindi mmoja katika nchi husika.

Awamu ya pili: Hii ndio fainali yenyewe. Washindi kutoka kila nchi husika, watapambana katika fainali hii.

Nchi sita za Afrika Mashariki na Kati zitahusika katika shindano hili, nazo ni: Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Fainali itatangazwa moja kwa moja katika matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC, kupitia kipindi chake maarufu - Dira ya Dunia, na pia kwenye mtandao bbcswahili.com.

 
 
VIUNGO VYA MTANDAO WA HAPA HAPA
Kuhusu Kimasomaso
29 Januari, 2009 | Vivutio
Shughuli za Kimasomaso
29 Januari, 2009 | Vivutio
Ukweli wa mambo
29 Januari, 2009 | Vivutio
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha