http://www.bbcswahili.com

19 Mei, 2008 - Imetolewa 16:52 GMT

Ingia bbcswahili.com kwa kutumia kiungo cha RSS

BBC World Service sasa inatoa viungo mbalimbali vya RSS kwa idhaa zake nyingi ikiwemo bbcswahili.com

viungo vya RSS ni nini?

Viungo vya RSS ni njia rahisi kwako kuweza kupata habari moto moto na taarifa mbali mbali kutoka bbcswahili.com

Wakati habari na vipindi mbali mbali vikiwa vinabadilishwa kila siku katika bbcswahili.com, Viungo vya RSS navyo vitakuwa vikibadilishwa kwa kutumia kisoma habari chako cha RSS. Katika kisoma habari chako cha RSS utaona vichwa vya habari vya karibuni kabisa, ikifuatiwa na muhtasari wake, na kiungo cha kukupeleka katika habari yenyewe.

bonyeza hapa kwa msaada na maelezo zaidi.l

Chagua kisoma habari cha RSS unachotaka kupokea habari kutoka bbcswahili.com kupitia chaguo mbali mbali zilizoorodheshwa hapo chini : Tafadhali tambua kwamba: ukibonyeza katika kisoma habari chochote cha RSS basi utashawishiwa kupakua faili la rdf.msaada

Nawezaje kujiunga na kisoma habari cha RSS kutoka bbcswahili.com?
Nawezaje kupata kisoma habari cha RSS?
Kwa kutumia bbcswahili.com kwenye tovuti yako


Nawezaje kujiunga na kisoma habari cha RSS kutoka bbcswahili.com?

Utahitaji kupata programmu inayoitwa RSS News Reader. Programu hii inaonyesha habari na maelezo kutoka katika tovuti uliyochagua katika kompyuta yako.

Unaweza kujiunga na kiungo cha RSS kwa njia mbali mbali zikiwemo:

NB: Visoma habari vipya vya RSS vitakujulisha iwapo unaweza kujiunga na RSS za BBC wakati ukitembelea tovuti hiyo.


Nawezaje kupata kisoma habari cha RSS?

Kuna visoma habari tofauti vya RSS vinavyopatikana. Utapata maelezo zaidi ya visoma habari hivi kwa kutafuta katika mtandao. Mara nyingi unaweza kuvipakua bure.

Visoma habari tofauti vya RSS vinafanya kazi katika mifumo tofauti ya kompyuta, hivyo unahitaji kuzingatia hili wakati ukifanya maamuzi yako.

Pia, ni muhimu kutambua kwamba baadhi ya visoma habari haviwezi kutambua baadhi ya lugha.


Kutumia viungo vya RSS toka bbcswahili.com katika tovuti yako.

Tunahimiza matumizi ya viungo vya RSS toka bbcswahili.com mradi tu masharti na sheria zetu zinazingatiwa:

masharti na taratibu

Hata hivyo tunataka kuona muundo muafaka unatumika na maelezo kwamba habari zinazotumia zinatoka BBC mara zote zinapotumiwa. Maelezo hayo lazima yaseme ''idhaa ya kiswahili ya bbc'' au ''Kutoka idhaa ya kiswahili ya BBC'' kwa vile itakavyofaa. Huruhusiwi kutumia nembo ya BBC au alama nyingine ya BBC.
Tuna haki ya kuzuia usambazaji wa habari na taarifa za BBC. Tafadhali soma masharti na taratibu zetu kwa maelezo zaidi.

BBC haihusiki na athari zozote zitakazojitokeza katika viungo vya RSS. Tafadhali soma masharti na taratibu zetu kwa maelezo zaidi.