Sera za mahusiano ya ndani na uhamiaji

Utangulizi: Mahusiano ndani ya jamii na uhamiaji

Ukaguzi wa pasi katika mojawapo ya mipaka ya Uingereza.
Image caption Vyama hivyo vitatu vinatofautiana sana kuhusu njia muafaka ya kupokea na kukaribisha raia wa kigeni wafanye kazi nchini Uingereza.

Je mkakati wa Uingereza juu ya suala la uhamiaji uwe wa namna gani? Wapo wanaoamini kuwa uhamiaji unaimarisha uchumi na umechangia kuifanya Uingereza ionekane kuwa jamii yenye uttamaduni wa aina mbali mbali.

Lakini pia wapo wanaosema kuingia kwa wahamiaji wengi kumechangia kuongeza shinikizo katika huduma za jamii kama vile afya, elimu na usafiri katika baadhi ya maeneo na imechangia kuwa na jamii ambayo imegawanyika

Vyama vikubwa zaidi vinaahidi hatua kali zaidi za kudhibiti mipaka ya Uingereza.

Conservative

• Kupunguza idadi halisi ya wahamiaji kufikia viwango vya miaka ya 1990 • Kuhakikisha kuwa wahamiaji wanaoweza kuleta mchango mkubwa katika uchumi ndiyo pekee wanaoruhusiwa kuingia Uingereza. • Kuunga mkono sera ya chama cha Labour ya mfumo wa pointi kwa wahamiaji, lakini pia kuweka mipaka katika idadi ya wahamiaji kwa mwaka toka katika nchi zisizo katika Umoja wa Ulaya • Kuunda jeshi la polisi la kukagua mipaka ya nchi likiwa na uwezo wa kusimamisha, kukagua, kuzuia na kukamata • Kutumia vidhibiti dhidi ya wahamiaji pale nchi mpya zinapojiunga na Umoja wa Ulaya • Kulazimisha mtihani wa lugha ya Kiingereza kwa yeyote anayetaka kuingia Uingereza kwa ajili ya kuoa au kuolewa. • Kufuatilia matumizi mabaya ya viza za wanafunzi. • Kuunga mkono vikundi vya kijamii ili kuondokana na umasikini kwa kuzingatia matokeo mazuri ya jitihada zao na si kwa kuzingatia imani ya kidini au asili(rangi) • Kuimarisha mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa wahamiaji.

Labour

• Kuendelea kuweka mbano katika mfumo mpya wa pointi kwa wahamiaji • Kuunga mkono kazi za Wakala wa kukagua viwanja vya ndege na bandari • Kuendelea kutoa fedha kwa vidhibiti vya elektroniki vya kuhesabu watu wanaoingia na kutoka Uingereza. • Kupanua mfuko wa fedha wa athari za uhamiaji (Migration Impacts Fund) ili kupeleka fedha katika maeneo ya nchi yanayopokea zaidi wahamiaji. • Kuleta mfumo mpya wa vitambulisho kwa raia wa kigeni • Kuendelea kusisitiza waajiri kutangaza nafasi za kazi zenye kuhitaji utaalam na ujuzi katika vituo vya kazi wiki nne kabla ya kuteua mfanyakazi mwenye ujuzi kutoka nje ya Umoja wa Ulaya. • Kuhakikisha wahamiaji wanapitia majaribio magumu ya lugha ya kiingereza kabla ya kuwasili Uingereza. • Kuondoa uwezekano wa kupata uraia au kuweza kuishi na kutulia Uingereza kunakosababishwa na kigezo cha kuishi kwa muda fulani.

Liberal Democrats

• Kuunda Jeshi la kukagua mipaka lenye mamlaka ya kipolisina kurudisha tena ukaguzi kwa wanaondoka. • Kutathmini mahitaji na nyenzo/rasilimali za mikoa ikiwa ni sehemu ya mfumo wa pointi kwa wahamiaji. • Kuunga mkono sera ya pamoja ya Ulaya juu ya suala la hifadhi kwa wakimbizi • Kuruhusu wakimbizi wanaotafuta hifadhi kufanya kazi • Kukomesha kuwekwa katika kizuizi kwa watoto katika vituo vya kizuizi • Kuongeza gharama za vibali vya kufanya kazi kwa waajiriwa wahamiaji ili kugharamia mafunzo kwa wafanyakazi wa kiingereza • Kutengeneza uwezekano wa kupata uraia kwa kwa wahamiaji walioishi Uingereza kwa miaka kumi kwa kuzingatia kufanikisha vigezo fulani • Kupitia upya sera za ugawaji wa makazi ili kuhakikisha huduma nzuri na usawa • Kuweka wakala huru wa hifadhi ya wakimbizi ili kuboresha maamuzi juu ya hifadhi na kupunguza rufaa. • Kuweka sera mpya ya kutoonesha jina katika maombi ya kazi ili kuondoa ubaguzi