Juhudi zaidi kupambana na Ukimwi-UN

Mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukimwi (UNAID)unasema kuwa takriban watu milioni sita na nusu katika mataifa machanga wanatumia tiba dhidi ya Ukimwi likifahamu kwamba wapo wengine milioni tisa wanaohitaji dawa bila ya kuwa na uwezo wa kupata dao hiyo.

Haki miliki ya picha 1
Image caption kuepuka gharama baadaye

Suala la tiba limezuka kuwa suala nyeti tangu majaribio ya mwezi uliopita kuonyesha kuwa unapotumia dawa mapema inasaidia na vilevile kuna uwezekano wa kutoambukiza wengine.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Tiba ni muhimu

Shirika hilo linakadiria hadi watu milioni 34 wanaishi na virusi huku ni watu milioni 30 waliofariki tangu maradhi haya yagunduliwe tareh 5 juni mwaka 1981.

Ingawa kiwango cha maambukizi kinashuka, mpango wa Umoja wa Mataifa una wasiwasi juu ya kupunguwa kwa uwekezaji katika kupambana na janga la ukimwi tangu mwaka jana.

Shirika hilo limeonya kua endapo hali hiyo itaendelea hivyo basi gharama zinazotokana na maradhi hayo zitakuwa kubwa zaidi baadaye.

Onyo hili linatokea wakati viongozi wa serikali mbalimbali wanajiandaa kwa mkutano wa kujadili ukimwi wiki ijayo mjini New York.