matumaini yapo kutibu saratani

Kuna uwezekano wa kuendeleza faida za dawa ya saratani kwa kuzuia kujitokeza kwa uvimbe kugeuka kuwa sugu kwa dawa hizo, wanasema wataalamu.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida liitwalo Science Translational Medicine, imedhihirika kuwa kila maradhi yanapozowea dawa hutokea hali ya mchanganyiko na kuongezeka kwa viwango vya kemikali kupinga dawa hizo mwilini.

Haki miliki ya picha Other
Image caption saratani

Wataalamu wanasema kuwa dawa iliyopo kwenye soko yenye uwezo wa kupambana na hali nzima ya saratani. Shirika la kupambana na saratani hapa Uingereza, yaani Cancer Research UK linasema kuwa hali hiyo inaleta ''matumaini makubwa''.

Kundi la wataalamu limekua likifanya ukaguzi wa dawa ya saratani aina cetuximab'', hii ikitumiwa kutibu saratani ya mkundu, kichwa na shingo pamoja na saratani nyingine zinazoathiri mapafu.

Dawa hii hulenga sehemu ya mapokezi ''EGFR'' inayosaidia katika kukuza mfano nywele ikiwa ni aina ya proteni ambayo badala yake hukuza uvimbe.

Wataalamu hao wanasema kuwa mwishowe miili ya wagonjwa wote itakua sugu kwa dawa hii ya cetuximab" na hapakua na elimu yoyote kuhusu jinsi hali hiyo ya miili lkukataa dawa ilivyoanza.

Majaribio yalionyesha jinsi selli zilivyokwenda kama magari yanapokuwa kwenye foleni -barabara inapofungwa bila njia mbadala.

Katika hali hii, uvimbe ulipanda na kuchukua njia ya EGFR na badala ya njia hii na kutumia moja ambayo huhusisha proteni tofauti ya ERBB2 na hivyo kuendelea kukua.

Dr Pasi Janne, kutoka taasisi ya Dana-Farber ya Boston, amesema kuwa proteni hii "ERBB2 huamsha njia mpya ambayo kwa kawaida haifungwi na dawa cetuximab, na kwa njia hiyo hupoteza muelekeo, kazi na sababu za dawa cetuximab.

"sababu dawa cetuximab haidhuru proteni ERBB2, bali pia ni njia rahisi inayoifanya saratani kuwa sugu kwa baadhi ya dawa".

Wataalamu hao wanasema kuwa kuna dawa nyingine zinazolenga proteni hiyo ERBB2 na ambazo tayari zimeisha idhinishwa kwa hiyo utafiti wa hivi sasa unaweza kutumika katika kuunda tiba nyingine muhimu".

Hata hivyo wataalamu hao wameonya kuwa uwezekano wa saratani kupata maarifa ya kukwepa dawa ni mkubwa.

Henry Scowcroft, Meneja wa habari za sayansi wa taasisi ya utafiti wa saratani Uingereza anasema kuwa, kwa bahati mbaya uvimbe unaweza kukataa tiba ya dawa, na kuelewa sababu ya kwanini haya yanatokea kimekua kigezo kikubwa kwa wataalamu.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Matiti yenye saratani

"utafiti huu mpya ni mfano mzuri wa jinsi wataalamu wanavyozidi kupiga hatua katika kugundua ujanja uliotumiwa na seli za saratani zinavyokwepa tiba, na kutafuta njia za kuzuia tabia hiyo ya kukwea tiba.

"utafiti kama huu unatupa mwangaza na matumaini makubwan kwamba tumefika kwenye kilele cha uhakika wa mabadiliko ya saratani, ingawa bado kuna kazi kubwa ya kuhitimisha kazi hii hadi ifanikiwe kikamilifu.