Athari za mpango wa uzazi wa IVF

Haki miliki ya picha none

Mpango wa uzazi ujulikanao kama IVF ama uzazi wa kutegemea sindano umehusiashwa na kuzuka kwa uvimbe katika fuko la uzazi baadaye katika maisha ya mtumiaji.

Wanawake wanaopewa dawa ya kurutubisha mayai ya uzazi waligunduliwa kuwa na uwezkano mkubwa wa kupata uvimbe wa kizazi ambao unaweza kugeuka kua saratani, wanasema wataalamu wa Uholanzi.

Hata hivyo athari zilizojitokeza ni ndogo sana, wanasema wataalamu.

Shirika la kujitolea linalotoa huduma kuhusiana na saratani linasema kua idadi iliyoshiriki katika utafiti huo uliochapishwa katika jarida lijulikanalo kama 'journal Human Reproduction'', ilikua ndogo mno kuweza kutoa takwimu za uhakika.

Wakati wa utafiti walitumia wanawake 25,000 waliohudhuria zahanati za kutafuta uzazi kwa kurutubisha huko Uholanzi mnamo miaka 1980 na 1990.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption mpango wa IVF

Uchunguzi uliofuata uligundua kua idadi kubwa ya wanawake walioathirika kwa uvimbe wa kizazi ilikua kubwa kuliko ilivyodhaniwa.

Ongezeko kubwa lilikua katika mfano mmoja wa uvimbe ambao mara kwa mara hugeuka kua saratani. Ingawaje aina hii haina makali sana kuliko aina nyingine ya uvimbe wa kizazi huhitaji kufanyiwa upasuaji.

Kwa mujibu wa taasisi ya Uholanzi inayoshughulikia saratani, mjini Amsterdam mwanamke mmoja kati ya wanawake 1,000 huathirika ingawa iligunduliwa kua idadi ya wanawake 3.5 kati ya 1,000 waliofanyiwa urutubishaji wa kizazi. Ongezeko la kiwango kidogo la uvimbe wa kizazi lilipatikana pia. Kwa ujumla kiwango cha saratani ya kizazi kiliongezeka kwa wanawake waliotumia mfumo wa kurutubisha uzazi, walisema wataalamu.

Prof Flora van Leeuwen, mhariri wa utafiti huo aliiambia BBC kua hatari ni ndogo mno. Lakini kuna ongezeko la hatari ya kuzuka kwa uvimbe usiopona ambao unahitaji tiba ya upasuaji.

"wanawake yafaa wafahamishwe kuhusu hili na athari zake ila athari na hatari zisitiwe chumvi.

Mipango inafanywa kwa uchunguzi zaidi kuthibitisha utafiti huu kwa kutumia washiriki wengi zaidi na kuchunguza kama wanawake wengi wanakabiliwa na hatari ya saratani.

Hata hivyo kuna ushauri kwamba "wanawake wanaweza kupunguza hatari ya saratani ya kizazi kwa kujihadhari uvutaji sigara na wajitahidi kupunguza uzani wao, na wanawake ambao wametumia tembe za kuzuia mimba au walioshika mimba hawana sababu ya kua na wasiwasi.