Wataalamu wafasiri vinasaba vya Sokwe

Vinasaba vya sokwe Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Vinasaba vya sokwe

Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge wamefasiri vinasaba vya sokwe. Vinasaba vya Sokwe ndiyo vya mwisho katika familia ya nyani kuorodheshwa.

Katika taarifa yao katika Jarida la masuala ya Sayansi,Nature, wataalamu hao wamesema kua kwa mara ya kwanza makundi ya watafiti kutoka maeneo yote duniani yanaweza kuchunguza tafauti baina ya sokwe,sokwe-mtu, nyani na aina ya nyani kama Orang-utans ili waanze kufahamu ni jinsi gani vijinasaba vya wanyama hawa vilivyogawanyika na kusababisha sisi binadamu kubuni lugha, utamaduni na sayansi.

Binadamu wamo kwenye fungu la Nyani mkuu kibayolojia. Chembechembe zetu ni takriban asili mia 98 sawa na sokwe,sokwe-mtu na orang-utans. Lakini tofauti ndogo katika vinasaba vyetu ndio sababu tuliweza kubuni sanaa, sayansi na utamaduni- nyani wenzetu hawakuweza kufanya hivyo.

Baada ya kukamilisha kufasiri vinasaba vya sokwe, sasa wataalamu wanaweza kuorodhesha chembechembe zote za nyani wakuu wote - na hivyo, kwa mujibu wa Dkt.Richard Durbin wa taasisi ya Sanger ya Chuo Kikuu cha Cambridge, tunaweza sasa kuanza kuelewa mpangilio wa jeni au(mpangojeni) kilichomfanya binadamu kuwazidi nyani wengine.

Haki miliki ya picha PA

Dkt.Durbin anasema: Nahisi kua katika kipindi cha miaka kumi au ishirini ijayo tutaweza kupata ufahamu wa ndani kabisa wa viini vinavyomfanya binadamu wa leo na hilo pia kutuwezesha kuelewa kilichotokea katika historia yetu ya kubadili jeni zilizoathiri ubongo na vifaa vingine vya mwili ndipo tuweze kufahamu kilichotufanya kile tulicho leo.

Uchungiz wa kwanza wa sokwe umeonyesha kua sisi tulijitenga kutoka sokwe takriban miaka milioni kumi iliyopita- mapema zaidi ya baadhi ya wataalamu walivyodhani. Kuna kitu ndani ya sokwe ambacho kinamzuia asiathirike na hali ya upungufu wa uwezo wa akili na mwili na hilo litawaezesha wataalamu kupata tiba ya hali hio.

Pamoja na hayo zawadi kuu kwa jamii ya watafiti ni kugundua kinachomfanya mwanadamu kua wa kipekee kama binadamu.