Afrika ina chemchemu ya maji ya kutosha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wengi wanahangaika kupata maji Afrika

Wanasayansi wanasema Afrika ambayo inajulikana kuwa ni bara kavu imekalia chemchemu kubwa ya maji.

Wanasema kwamba maji yanayopatikana katika chemchemu za chini ya ardhi yanapita mara 100 ya maji yanayopatikana juu ya ardhi.

Jopohilola wanasayansi limechapisha ramani kamili ya kiwango cha hazina hii iliyofichika.

Wanasanyasi hao walioandika utafiti huu kwenye jarida la Utafiti wa Mazingira, [Environmental Research Letters] wanasisitiza kwamba uchimbaji visima kwa wingi huenda isiwe njia muafaka ya kuongeza vyanzo vya maji.

Katika bara zima la Afrika inasemekana zaidi ya watu millioni 300 hawana uwezo wa kupata majisafiya kunywa.

Mahitaji ya maji yanatazamiwa kuongezekasanakatika miongo ijayo kutokana na kuongezeka kwa watu duniani na mahitaji ya kilimo cha umwagiliaji maji ili kukuza mazao.

Afrika

Maji ya maziwa namitohutegemea misimu ya mafuriko na ukame na vinaweza kuathiri kupatikana kwake kwa watu na kilimo. Kwa sasa ni asilimia 5 tu ya ardhi yenye rutuba humwagiliwa maji.

Na sasa kwa mara ya kwanza wanasayansi wameweza kufanya tathmini ya maji yaliyofichika katika chemchemu kwa bara zima la Afrika. Watafiti kutoka taasisi ya uchunguzi wa jiologia ya Uingereza na chuo cha Kikuu cha London (UCL) wameratibu kwa kina kiwango cha chemchemu hizi za chini ya ardhi kwa bara zima.

Helen Bonsor aliyeshiriki katika utafiti huo anasema hadi hivi sasa maji hayo yalikuwakamaile hadithi ya "hayuko machoni hayuko moyoni" . Ana matumaini kwamba ramani mpya zitafungua macho ya watu kuhusu hazina hiyo.

"chemchemu kubwa zaidi iko kaskazini ya Afrika katika mabonde ya Libya,AlgerianaChad," alisema.

Matukio ya Kale

Kutokana na mabadiliko katika hali ya hewa ambayo yameligeuza eneo laSaharakuwa jangwa katika kipindi cha karne nyingi ,chemchemu nyingi za chini ya ardhi zilijazwa maji mara ya mwisho miaka 5,000 iliyopita.

Haki miliki ya picha online
Image caption Chemchemu za maji Afrika na viwango vyake

Hata hivyo wanasayansi wanatoa tahadhari kuhusu njia bora zaidi ya kuyapata maji hayo.Wanasema kuchimba visima kwa wingi huenda kukukaathiri chemchemu hizo na kusababisha upungufu mkubwa wa maji. Wanapendekeza mbinu mbadala ambazo zitahakikisha vyenzo endelevu.