Makahaba na michezo ya Olimpiki London

Image caption Makahaba barabarani

London 2012: Je michezo ya Olimpiki italeta makahaba zaidi?

Kabla ya kuanza kwa msimu wa michezo ya kimataifa mfano kombe la dunia na michezo ya Olimpiki kwa kawaida, kitu ambacho huanza utakisikia kwanza na zaidi ni hofu ya ongezeko la biashara ya ukahaba pamoja na tahadhari ya biashara haramu ya ngono. Hofu hii inatokea kwa sababu ya ongezeko la watu. Lakini je, biashara ya ukahaba itaongezeka kweli kwa sababu ya michezo ya olimpiki 2012?

Inaonekana kama kila wakati shindano la kombe la dunia au michezo ya olimpiki inapokaribia, bila shaka ndipo tahadhari kutoka kwa vyombo vya habari vya kimataifa, mawaziri wa serikali na hata polisi nazo zinapoongezeka.

Wote huelezea hofu kuwa maelfu ya wanawake watauzwa katika biashara ya ukahaba hadi katika taifa mwenyeji ili kukidhi mahitaji ya kingono ya makundi ya watu wanaowasili nchini humo.

Ujumbe sawa na huo umekuwa ukitolewa kuhusiana na michezo ya Olimpiki 2012 mjini London.

Mwezi Januari mwaka 2010, aliyekuwa waziri wa michezo ya Olimpiki katika serikali iliyopita, Tessa Jowell, aliambia wabunge kuwa "michezo ya kimataifa wakati mwingine inaweza kufanya biashara ya ngono kukithiri na jambo hili halikubaliki. Nitajitolea kuhakikisha kuwa wanaoendesha biashara hizo hawatumii michezo ya London kwa manufaa yao."

Dennis Hof, anayemiliki jumba kubwa sana la makahaba la Moonlite Bunny Ranch, lililoko mjini Nevada, Marekani, anasema kuwa London ijiandae kwa wasichana 1,000 wataoletwa nchini humo kwa sababu ya biashara za ngono kutoka kusini mwa kanda ya Asia Mashariki, Albania na barani Afrika. Wote wataletwa na makundi yanayohusika na uhalifu pamoja na biashara ya mihadarati.

Image caption Makahaba

Hof, anayetaka aruhusiwe kuendesha jumba halali la biashara ya ngono mjini London wakati wa michezo hiyo, anasema kuwa utabiri wake umejikita katika kile alichokiona wakati wa michezo ya olimpiki ya mwaka 2010 mjini Vancouver, Canada.

Je onyo hizi zina uhakiki?

Michezo ya Olimpiki, mwaka 2004 mjini Athens, ndio ilionekana kuwa michezo ya kwanza ya kimataifa kuzua hisia hizi baada ya kuelezewa hofu juu ya ongezeko la makahaba. Mji huo ulielezea kuona ongezeko maradufu la biashara ya ngono.

Hata hivyo ripoti ya shirika la kimataifa dhidi ya biashara haramu na ulanguzi wa wanawake, (GAATW), inaonyesha kuwa idadi ya visa hivyo mjini Athens mwaka 2004 iliongezeka hadi watu 181, kutoka kwa 93 mwaka 2003.

Kabla ya kuanza kwa dimba la kombe la dunia nchini Ujerumani mwaka 2006, onyo kama hizi zilitolewa na vyombo vya habari na maafisa wengine wakuu lakini kulingana na ripoti iliyotolewa na Muungano wa Ulaya kuanzia Januari mwaka 2007, serikali ya Ujerumani ilipata tu visa vitano vya ukahaba vilivyohusishwa na dimba hilo.

Ripoti hiyo ilisema kuwa ongezeko la biashara haramu ya ngono pamoja na ulanguzi wa watu kwa sababu ya kutumiwa kwa faida za kingono, wakati wa kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani haikutokea kama ilivyokuwa imehofiwa. Na kwamba madai ya makahaba 40,000 kuingia nchini humo hayakuwa ya kweli kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari.

Ili hali kombe la dunia la mwaka 2006, limetumiwa kama mfano wa kuonyesha namna ambavyo idadi kubwa ya makahaba walilipwa na idadi kubwa ya watu waliohudhuria dimba hilo kwa mahitaji yao ya kingono.

Tukisalia katika kombe la dunia, utafiti uliofadhiliwa na shirika la umoja wa mataifa la kukadiria idadi ya watu, UNFP, iliyofanywa nchini Afrika Kusini wakati wa kombe la dunia mwaka 2010, iligunduliwa kuwa hapakuwa na tofauti kubwa katika ongezeko la wanaume waliotafuta huduma za makahaba wakati wa mchuano huo.

Haki miliki ya picha
Image caption Majumba ya makahaba kwa picha

Lakini kulikuwa na wasiwasi kuwa kati ya makahaba 40,000 na 100,000 kutoka kote duniani wangeingia nchini humo kwa sababu ya shindano hilo.

Utafiti huo unasema kuwa licha ya taarifa za vyombo vya habari kabla ya michezo hiyo , hapakuwa na ukweli wa kuongezeka kwa biashara ya ngono na kuongezeka kwa makahaba kama ilivyokuwa imetabiriwa.

Wengi sasa wanatumia mifano ya michezo ya olimpiki iliyofanyika nchini Ugiriki, Ujerumani na Afrika Kusini kusema kuwa London bora ijitayarishe kwa ongezeko la makahaba.

Tayari kundi moja linalowakilisha makahaba mjini London, x:talk, lmetoa wito kwa polisi kukoma kuwakamata, kuwazuia au kuwarejesha makwao watakaokamatwa hadi michezo hiyo ya Olimpiki iishe.

Msemaji wa kundi hilo ansema kuwa pia msako wa polisi dhidi ya maumba ya makahaba hasa mashariki mwa London inasbabisha makahaba kutorokea kwingineko kutoka kwa mashirika yanayowasaidia makahaba hao na hata vituo vya afya , na hivyo kusababisha wito wa kuwataka polisi kukoma kuwakamata makahaba.