Mti wa Moringa afueni ya chakula Niger

Imebadilishwa: 14 Juni, 2012 - Saa 16:04 GMT

Mradi wa Moringa

  • Kitu kipya kinajitokeza katika upembe mmoja ambao ni kame magharibi mwa Niger. Mmea wa ajabu wa Moringa ndio umeanza kuwa kama silaha ya kupigana na njaa ambayo hujitokeza katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika mara kwa mara.
  • Miaka miwili imepita sasa baada ya baana la njaa kukumba nchi hiyo, mimea haikukomaa na watu milioni 5.4 wanakabiliana na hali ngumu kupata chakula. Takriban watu milini 18 katika kanda hiyo wanakabiliwa na njaa.
  • Akina mama kama Fatimata Birmay kutoka mkoa wa Tillaberi, wamelazimika kuwapeleka watoto wao kupokea chakula cha msaada wakiwa katika hali mbaya.
  • Mti wa Moringa, huenda ikawa suluhu kwa watu kama bi Birmay wakati ikikuwa katika mazingira mabovu ya Niger. Majani ya mti huu yanaweza kutumika kama chakula na yana madini ya vitamini A na B.
  • Mti huu ulitumiwa kitamaduni kama chakula na hata kwa faida zake za kimatibabu, lakini ufahamu huo uliwapotea watu baada ya miaka mingi. Na sasa kikundi cha akina mama 52 wameamua kuupanda mti huu kuweza kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula kwa familia zao.
  • Bi Hama anasema kuwa mamake aliamua waanzishe mradi huu wa upanzi wa mti wa Moringa , kwa sababu watu waliikuwa wanateseka kwa ukosefu wa chakula.
  • Kikundi hiki cha akina mama kilikuwa makini kuanzisha mradi huu wa Moringa kwa sababu mmea utakuwa tayari kutumiwa kama chakula katika muda wa miezi miwili tu
  • Pia kuna chakula kingine wanachopanda na mama Hama anasema mradi umemwezesha kuuza na kupata faida kubwa.
  • Mama Hama anasema njia anayopenda kupika Moringa ni kwa kuiweka kwenye chungu, kuongeza mafuta, pilipili kidogo na kitunguu. Anasema ana furaha kwamba anaweza kujisaidia sasa.
  • Bwana Kimba anasema mwanzoni ilikuwa vigumu kueleza watu kuhusu manufaa ya mti huu na kwamba unaweza kutumika kama chakula

Akina mama katika kijiji kimoja nchini Niger, wameungana kuanzisha mradi wa upanzi wa mti wa Moringa ambao kuweza kuutumia kama chakula.

Akina mama hawa hulima, kuupanda na kupalilia mti huo ambao huwa tayari kutumika kama chakula katika miezi miwili tu.

Wengi hawakujua kama mti huu ungewza kutumika kwa namna hiyo kama mboga na sasa akina mama hao wanataka kuhakikisha kuwa wanakabiliana vilivyo na uhaba wa chakula.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.