Wakimbizi wameongezeka duniani

Haki miliki ya picha none
Image caption Wakimbizi kambini

Ripoti ya shirika la kuwahudumai wakimbzi la umoja wa mataifa imeonyesha hali ya wakimbzii mwaka 2011 kuwa mwaka ulioshuhudia ishughui nyingi katika mipaka ya nchi duniani huku wengi wakifanywa kuwa wakimbizi kuliko wakati wowote kuanzia mwaka 2000.

Ripoti hiyo kwa jina "Global Trends 2011" inaelezea kwa kina kwa mara ya kwanza ukubwa wa tatizo la watu kulazimishwa kuhama makwao kutokana na mizozo mingi tu, ikiwemo mzozo wa mwaka 2010 nchini Côte d'Ivoire na punde ulifuatiwa na mizozo mingine Libya, Somalia, Sudan na kwingineko.

Watu milioni 4.3 walipoteza makao yao huku watu 800,000 kati yao wakitoroka makwao na kuwa wakimbzii wapya.

"Mwaka 2011 ulishuhudia mateso makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa tena. Kwa maisha ya watu wengi kutumbukia katika hali mbaya katika kipindi cha muda mfupi ni jambo la kusikitisha na hii inaashiria hasara kubwa kwa waathirika" alisema kamishna wa shirika la UNHCR António Guterres.

"Tutashukuru sana lakini mfumo wa kimataifa wa kuwalinda watu kama hao, ulisimama imara wakati wa matukio hayo na kwamba mipaka ilisalia kuwa wazi. Hiki ni kipindi kigumu sana" aliongeza bwana Guterres.

Kote duniani watu milioni 42.5 mwaka jana walitumbukia katika maisha ya ukimbizi wengine milioni 15.42 wakiwa wakimbizi wa ndani au wengine milioni 26.4 wakiwa wanatafuta hifadhi

Licha ya idadi kubwa ya wakimbizi wapya, idadi kamili ilikuwa chini ikilinganishwa na mwaka 2010, ambapo watu milioni 43.7 walikuwa wakimbizi sababu kubwa ikiwa watu wengi walikuwa wanarejea nyumbani kutoka ukimbizini

Haki miliki ya picha
Image caption Wakimbizi nchini DRC

Ripoti hiyo ikitizamwa kwa msingi wa miaka kumi, inaonyesha matukio yaliyotia wasiwasi mkubwa. Cha kwanza ni kwamba watu wengi wanaathirika kutokana na ukimbizi kote duniani, takwimu za kila mwaka zikionyesha ni zaidi ya watu milioni 42 katika kila miaka mitano iliyopita.

Cha pili ni kwamba, mtu anayekuwa mkimbizi anasalia katika hali hiyo kwa miaka mingi, wakati mwingi akiwa amekwama kambini au akiwa anaishi maisha duni katika maeneo ya mijini.

Kati ya wakimbizi milioni 10.4 wanaofahamika na UNHCR, takriban milioni 7.1 ya wakimbizi hao wamekuwa uhamishoni kwa miaka mitano wakisubiri kujua hali yao.

Kwa ujumla, Afghanistan inasalia kuwa nchi inayotorokwa na watu wengi wanaoishia kuwa wakimbizi kisha kufuatiwa na Iraq, Somalia wkimbizi milioni 1.1, Sudan watu laki tano na hatimaye DRC watu efu 491,000. Wengi wa wakimbizi hao wamekimbilia Pakistan,Iran, Kenya na Chad.