Wanariadha hodari wa Afrika

Image caption Wanariadha hodari wa Afrika

Wanariadha kutoka nchi 53 za Afrika, wamekuwa wakiwasili mjini London kabla ya sherehe za ufunguzi rasmi wa michezo ya Olimpiki mwaka 2012.

Sasa nani miongoni mwa wanariadha wa barani Afrika ni washindani wakubwa wa medali ya dhahabu?

Segun Toriola - Nigeria: Mchezaji wa Table tennis

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Segun Toriola

Segun Toriola ndio mchezaji bora zaidi wa Table Tennis barani Afrika. Anashiriki michezo ya Olimpiki kwa mara ya sita sasa. Michezo yake ya kwanza ya Olimpiki ilikuwa ya Barcelona mwaka 1992.

Miaka minne iliyopita katika michezo ya olimpiki ya Beijing, alikuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika kuwahi kufika robo fainali.

Kitindamimba katika familia ya watoto tisa, yeye hucheza michezo ya kulipwa nchini Ufaransa.

Bingwa wa zamani wa michezo ya jumuiya ya madola, amefanikiwa kushinda kila shindano kubwa barani Afrika na kuwa mchezaji bora zaidi kwa karibu miaka ishirini.

Lakini akiwa na umri wa miaka 38, mjini London mwaka huu huenda ikawa michezo yake ya mwisho ya olimpiki.

Benjamin Boukpeti - Togo: Mpiga makasia

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Benjamin Boukpeti

Medali ya shaba aliyoshinda Benjamin Boukpeti katika michezo ya Olimpiki mjini Bijing katika mashindano ya wanaume mtu mmoja mmoja, ilikuwa medali ya kwanza ya olimpiki katika historia ya Togo.

Alikuwa mwanaume wa kwanza mwafrika mweusi kushinda medali katika shindano la slalom.

Benjamin alizaliwa nchini Ufaransa kwa mama mfaransa na babake raia wa Togo.

Amekuwa akikabiliana na majeraha tangu kushiniriki mashindano Beijing, lakini sasa atashiriki kwa mara ya tatu sasa michezo ya olimpiki kwa matumaini makubwa.

Kirsty Coventry - Zimbabwe: Mwogoleaji.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kirsty Coventry

Kirsty Coventry anashikilia rekodi ya mita 200 ya uogeleaji ya backstroke, na katika mashindano yake mara mbili katika michezo ya olimpiki ameshinda medali mbili za dhahabu, shaba nne na fedha moja.

Kirsty mwenye umri wa miaka 28 ni mpambe wa Zimbabwe na anajulikana kama "msichana wetu wa dhahabu" kwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe. Ametajwa kama mwogeleaji bora zaidi barani afrika mara tano.

Sifiso Nhlapo - Afrika Kusini: Mwendesha baisikeli ya BMX

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Sifiso Nhlapo

Mshindi wa zamani wa fedha na shaba katika mashindano ya ubingwa wa dunia, Sifiso Nhlapo amewakilisha Afrika Kusini kwenye mashidano ya ubingwa wa dunia mara tisa.

Akiwa mjini Beijing - wakati mashindano ya baisikeli ndio yalianza kushirikishwa kwenye Olimpiki, nusura kupata medali ya dhahabu lakini kwa bahati mbaya akabanduliwa nje. Ingawa aliweza kufika fainali.

Mwaka uliofuata, alipata jeraha la shingo kwenye ajali, lakini mwili wake ukawa bado una nguvu. Bila shaka ni mmoja wa wale ambao watu watakuwa wanawatizama.

Aya Medany - Misri: Kushiriki mashindano matano (Modern pentathlete)

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Aya Medany

Baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika michezo ya Olimpiki mjini Athens mwaka 2004, akiwa tu na miaka 15, Aya Medany sasa ndio mchezaji anayetambulika zaidi kuliko wote nchini Misri.

Mchezo wake wa modern pentathlon - yeye hufanya kuogelea, kuendesha farasi, Kukimbia na kulenga shabaha

Kama muisilamu, dini yake inamtaka afanye hayo yote akiwa amevalia mavazi maalum.

Ni mchezaji pekee ambaye hufanya hayo yote akiwa amejifunika kichwa chake.

Michezo ya London 2012 ni michezo yake ya tatu ya Olimpiki na sasa analenga kuimarisha mchezo wake na kuwa bora kuliko nafasi ya nane aliyokuwa katika michezo ya Beijing.

Caster Semenya - Afrika Kusini: Mkimbiaji wa mita 800

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Caster Semenya

Wakati Caster Semenya aliposhinda ubingwa wa dunia, mwaka 2009, kulianza kuzuka tetesi kuhusu jinsia yake ikiwa ni mwanamke au mwanaume.

Lakini licha ya kupata wakati mgumu kuweza kufanya vyama kama alivyofanya mnamo mwaka 2009 katika mbio za mita 800, amechukua muda mrefu kurejelea hali yake ya kawaida ili angalau kuweza kuvunja rekodi ya mbio hizo ambayo haijawahi kuvunjwa tangu mwaka1983.

Hii ni mara yake ya kwanza kushiriki michezo hiyo ya Olimpiki

Na sasa bingwa wa zamani wa olimpiki wa mbio hizo, Maria Mutola akiwa kocha wake, bila shaka yuko kwenye mikoni mizuri.

Tirunesh Dibaba - Ethiopia: Mkimbiaji wa mbio za mita 5,000 na mita 10,000

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Tirunesh Dibaba

Bingwa mtetezi wa mbio za mita 5,000m na 10,000, Tirunesh Dibaba anajulikana kama mwanamke mwenye kumaliza mbio zake kwa kasi zaidi katika mbio za masafa marefu.

Tangu michezo ya Olimipiki amekuwa akikabiliwa na majeraha kwa muda mrefu na kuwa sababu ambayo hajakuwa akikimbia kwa muda mrefu.

Lakini Hali yake inaonekana huenda atafanya vyema.

Dibaba anasubiriwa kutoana jasho na mu Ethiopia mwenzake Meseret Defar pamoja na Mkenya Vivian Cheruiyot.

Amantle Montsho - Botswana: Mkimbiaji wa mbio za mita 400

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Amantle Montsho

Bingwa wa mashindano ya nchi za jumuiya ya madola na bingwa wa Afrika, Amantle Montsho atakuwa analenga kupata medali ya kwanza ya michezo ya Olimpiki na kwake atakuwa anashiriki kwa mara ya tatu michezo hii ya Olimpiki.

Mjini Athens hakuweza kufuzu , mjini Beijing aliweza kufika fainali lakini mjini London ana matumaini ya kupata medali ya dhahabu.

Kasi yake inasemekana kuongezeka angalau tangu kushiriki kwake katika michezo ya Beijing inasemekana yeye ndiye atakuwa kizingikiti kikubwa kwa washidani wengine.

Mary Keitany - Kenya: Mkimbiaji wa mbio za Marathon.

Image caption Mary Keitany

Miaka mitatu iliyopita, Mary Keitany alisalia vinywani mwa wengi baada ya kushinda ubingwa wa dunia wa mbio za nusu marathon.

Aliweza kufuatiliza ushindi huo kwa kuvunja rekodi ya dunia katika mbio hizo, rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa.

Alimaliza wa tatu katika mbio za marathon za New York ingawa baadaye aliweza kushinda mbio za marathon za London na kuwa wa nne kuwahi kumaliza kwa kasi zaidi katika historia ya mbio hizo.

Ni kwa sababu ya ufanisi huu ndio anaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupata ushindi mjini Lond.

David Rudisha - Kenya:Mkimbiaji wa mbio za mita 800.

Image caption David Rudisha

Bingwa wa dunia na mwenye kushikilia rekodi ya dunia, David Rudisha amekuwa mbele katika mbio za mita 800 kwa miaka miwili iliyopita.

Mnamo mwezi Agosti, alivunja rekodi ya dunia mara mbili kwa wiki moja na kisha kushinda dhahabu mwaka jana katika mashinadno ya bingwa wa dunia nchini Korea Kusini.

Na mkenya huyo anaonekana kuwa na nafasi nzuri kushinda kwenye michezo hii.

Itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki michezo ya olimpiki , hakupata fursa kushiriki michezo ya Beijing kwa sababu ya jeraha.

Babake, Daniel, aliwahi kushinda medali ya shaba mjini Mexico mwaka 1968.