Mganda aridhika licha ya kushindwa

Ganzi Mugula alitumia miaka 12 ya matayarisho na kupata mda unaohitajika kufuzu ili kushiriki mashindano ya Olimpiki. Hatimaye alipofanikiwa na kuingia dimbwi mapema Alhamisi alikaa humo kwa mda wa sekunde 27.58.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kuogelea

Mugula ni mhandisi wa komputa anayefanya kazi mjini Kampala na Benki ya Stanbic, akiwa pia nahodha wa kikosi cha Uganda.

Alisema baada ya kumaliza shughuli dimbwini ''Nimefanikiwa kutimiza mda ule ule niliouweka mjini Shanghai kwenye mashindano ya Dunia.

Mbio za kutafuta fursa ya kufuzu kuwania medali za mita 50, zikiwa ndiyo fupi katika mashindano ya Olimpiki ndiyo yenye washiriki wengi wanaoingia kwa njia ya kubahatisha na washiriki wengi mno kutoka Mataifa ambayo kawaida hayana uhusiano na mashindano ya kuogelea.

Kwenye mashindano haya utakuta watu kutoka Benin, Jamhuri ya Afrika ya kati, Djibouti, Rwanda na Ethiopia pamoja na Mugula mwenye umri wea miaka 33.

Mugula huenda asirudi kushindana na mabingwa kama Mbrazil Cezar Cielo lakini ameweza kutumia dimbwi moja na kutimiza ndoto yake ya kushiriki Olimpiki na daima atakumbuka London 2012 kwa furaha.