Masumbwi ya akina mama

Elena Savelyeva alikua mwanamke wa kwanza kushinda pambano la kwanza kabisa kwenye mashindano ya Olimpiki la masumbwwi ya wanawake mbele ya halaiki ya watazamaji.

Siku hii ya jumapili vilevile mashindano ya Olimpiki yameshuhudia mchezo wa masumbwi wa wanawake kwa mara ya kwanza. Mashindano haya kwa leo yalipanga wanawake wanaoshindana katika uzani wa fly, light na middleweight.

Mapambano ya leo yalishuhudia pambano kati ya Mwanamke kutoka Urusi akishinda pambano la kwanza. Elena Savelyeva aliyemshinda Kim Hye-song wa Korea.

Savelyeva alishinda kwa pointi 12-9 victory was.

Hata hivyo Karlha Magliocco ambaye atapambana na Mrussi kwenye robo fainali alivutia sana ummati wa watu waliokuja kujionea masumbwi ya akina mama. Ukumbi ulichangamka tena alipoingia bingwa wa dunia wa mara tano kutoka India Mary Kom.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mary Kom wa India

Baada ya kushinda pambano lake kwa pointi 19-14 dhidi ya Karolina Michalczuk wa Poland Kom alitoa chozi la furaha na kumkumbatia mpinzani wake.

Machozi ya Kom alisema baadaye ni kuona juhudi zake za miaka mingi kutaka mchezo wa masumbwi kwa wanawake uruhusiwe kwenye mashindano ya Olimpiki.

Kom, ameongoza juhudi za kutaka mchezo wa kwa wanawake uwekwe kwenye orodha ya mashindano ya Olimpiki kwa wanawake.