Muogeleaji bora Duniani astaafu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Michael Phelps

Enzi ya kutawala ya mda mrefu katika fani ya mchezo wa kuogelea kwa bingwa asiye wa kawaida Michael Phelps kumefikia ukingoni kwenye mashindano ya London.

Phelps mwenye umri wa miaka 27, alionyesha umahiri wake pale alipoipiku timu ya Japan na kuweka rekodi ya ushindi wa medali ya dhahabu kwa mara ya 18.

Akishangiliwa na umati wa watu waliojitokeza kushuhudia mashindano hayo ya London Olympiki aliungana na Matthew Grevers, Brendan Hansen na Nathan Adrian katika ushindi huo.

Ikisaidiwa na Phelps, timu ya Marekani kwa urahisi waliweza kuifunika timu ya Japan na Australia katika tukio ambalo Marekani haijawahi kushindwa katika historia ya michezo ya Olympiki ya hivi karibuni, ukiondoa ile ya mwaka 1980 iliposusia ya Moscow. Katika fainali za mashindano hayo Wamarekani walitumia dakika 3 sekunde 29 nukta 35.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Phelps na medali zake

Siku ya Ijumaa Phelps alishinda medali yake ya dhahabu ya mara ya 17 aliposhiriki binafsi mashindano ya mita 100 butterfly, katika shindano alilofanya vizuri zaidi ya mashindano Olympiki mbili zilizopita.

Mwaka 2000 Phelps alishiriki kwa mara ya kwanza michezo ya Olympiki ya Sydney, na kuwa muogeleaje wa umri mdogo wa kwanza katika timu ya Marekani akiwa na umri wa miaka 15 akimaliza wa tano mashindano ya kuogelea-butterfly ya mita 200.

Mwaka 2001 alikuwa kijana mdogo wa kwanza akiwa na miaka 15 na miezi 11 kuweka rekodi ya dunia aliposhinda mita 200 butterfly.

Mwaka 2003 alishinda mashindano manne katika bingwa wa dunia mjini Barcelona na kuwa muogeleaji pekee katika historia kuweka rekodi za dunia katika mashindano tofauti kwa siku moja.

August mwaka 2004, alishinda medali 6 za dhahabu na mbili za shaba katika mashindano ya Athens Olympics baada ya kujaribu kuvunja rekodi ya Mark Spitz aliyekuwa na rekodi ya medali 7 za dhahabu.

Mwaka 2007 aliungana na Spitz kama muogeleaji pekee kushinda mashindano saba katika mashindano ya kimataifa ya kuogelea wakati wa mashindano ya bingwa wa dunia ya Melbourne nchini Australia.

Mwaka 2008 alivunja rekodi ya bingwa Spitz kwa medali 8 katika michezo ya Olympic mjini Beijing, akiweka rekodi saba za dunia na kuwa mtu mashuhuri wa kimataifa.

Mwaka 20011 alishinda medali nne za dhahabu katika mashindano ya bingwa wa dunia mjini Shanghai Uchina, lakini alizidiwa na Mmarekani mwenzake Ryan Lochte walipokutana katika mechi mbili ambapo Lochte alishinda dhahabu tano.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Phelps

Mwaka 2012 amefanikiwa kushinda medali nne za dhahabu na mbili za fedha katika michezo ya London Olympiki, anayosema itakuwa shindano lake la mwisho.

Phelps anaondoka akiwa na rekodi ya juu katika Olympiki ikiwa ni mara mbili zaidi ya mwingine yeyote yule akiwa na medali 18 za dhahabu na ujumla ikiwa ni medali 22, ikiwa ni medali nne zaidi ya yeyote yule katika mchezo wowote ule.