Wanawake wagombea kulipa laki 2.5

Imebadilishwa: 31 Agosti, 2012 - Saa 08:25 GMT

Sema Kenya

Tume ya uchaguzi, IEBC, imesisitiza kwamba ada itakayolipwa na wagombeaji viti vya mwakilishi wa wanawake wilayani, itakuwa ni shilingi elfu mia mbili na hamsini wala sio nusu milioni kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Kupitia taarifa iliyochapishwa magazetini, tume hiyo imekiri kwamba tangazo lake la hapo awali liliwavuruga wasomaji na kusababisha hofu kwamba wanawake wengi wangezuiliwa kugombea viti hivyo kutokana na ukosefu wa fedha.

“Kutokana na hayo, tume ingependa kusisitiza kwamba kosa hilo limebainika na tumependekeza kwamba wagombea viti vya mwakilishi wa wanawake wilayani walipe Sh250000 wala sio Sh500000,” tangazo hilo lilisema.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.