Wanamuziki wa Afrika watumbuiza mjini London

Imebadilishwa: 7 Septemba, 2012 - Saa 12:57 GMT

Treni ya 'The African Express' kwa picha

  • Treni hiyo yenye wanamuziki 80 kutoka barani Afrika, Ulaya na kwingineko duniani iko katika safari ya wiki moja nchini Uingereza. Hawa ni wacheza gita Amadou Bagayoko kutoka Mali na mwenzake Romeo Stodart wa bendi ya Uingereza ya Magic Numbers. Picha ni kwa niaba ya mpiga picha : Manuel Toledo BBC Africa
  • Safari hii ni sehemu ya mradi ulioanzishwa mwaka 2006, wakati mwanamuziki kutoka Uingereza, Damon Albarn wa bendi maarufu ya Blur and Gorillaz alishirikiana na mpenzi mwingine wa muziki wa Afrika,Stephen Budd
  • Baadhi ya magwiji wa muziki kutoka Afrika wakiwemo, Baaba Mal, Rokia Traore, Tony Allen na Bassekou Kouyate wako kwenye treni hiyo. Waliungana na wasanii wengine chipukizi.
  • Kuna ushirikiano mkubwa wa wanamuziki hao. Hapa Damon Albarn anapiga ala zake na wasanii Reeps One, African Boy, M.anifest, Pauli The PSM pamoja na Hama Sangare akipiga mboko na Jonny the Temper akipiga kigoma.
  • Mpiga ngoma mashuhuri wa Nigeria Tony Allen ameshabikiwa sana katika safari hii. Anasifika sana nchini Uingereza kwa sababu ya ushirikiano wake na Fela Kuti ambaye waliunda naye aina ya muziki wa Afrobeat.
  • Tamasha hili la The Africa Express ni sehemu ya tamasha la London 2012 ambalo limekuwa likiendelea sambamba na michezo ya Olimpiki na Paralympic. Mwanamuziki wa Senegal, Baaba Maal aliandaa Africa Utopia.
  • Ngoma tamu kutoka katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia zimesikika kwenye treni hiyo. Yote haya kwa niaba ya bendi ya mjini Kinshasa Jupiter & Okwess International.
  • Kila siku wasanii wa treni hiyo hufika katika shule na kumbi mbali mbali kucheza mzuki wao. Hapa mwanamuziki Rokia Traore, Romeo Stodart, Mamah Diabate, Diabel Cissokho na M.anifest wanapiga muziki katika kituo cha kurekodi muziki cha Leeds' Jumbo Records.
  • Msanii kutoka Afrika Kusini ambaye pia ni DJ, Spoek Mathambo - aliye kando ya dirisha- anaungana hapa na mwanamuziki wa Misri, Kareem Rush, kutoka kwa bendi ya Arabian Knightz, pamoja na msanii mwingine M1 kutoka kikundi cha wanamuziki wa Marekani Dead Prez.
  • Hadi kufikia sasa, wasanii walio kwenye treni hii wamefanya tamasha tatu kubwa mjini Middlesbrough, Glasgow na Manchester. Hawa hapa ni wasanii kutoka Tanzania Mim Suleiman, Mwanamuziki kutoka Mali Bassekou Kouyat, mpiga fidla Marques Toliver na Kyla La Grange kwenye Piano

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.