Yaliyojiri Afrika kwa picha

Imebadilishwa: 24 Septemba, 2012 - Saa 11:02 GMT

Picha za Afrika wiki hii

  • Kumekuwa na maandamano wiki iliyopita katika nchi nyingi zenye waisilamu wakipinga filamu iliyotengezwa nchini Marekani ikidhihaki uisilamu. Maandamano hayo yamefanyika Ijumaa iliyopita. Hawa ni waisilamu mjini Mombasa Kenya wakiiteketeza bendera ya Marekani kudhihirisha kero lao.
  • Mamia ya wanawake walimiminika barabarani mjini Lome, Togo, wakiwa wamevalia mavazi mekundu wakimtaka rais wao Faure Gnassingbe ajiuzulu. Wiki iliyopita wanawake hawa waliosusia ngono mwezi jana wakitaka rais Gnassingbe aondoke mamlakani. .
  • Siku hiyo hiyo, wafuasi wa upinzani nchini Guinea, wanawashangilia viongozi wao wakitaka kampuni moja ya Afrika Kusini nchini humo ambayo imepewa mkataba wa kudurusu sajili la wapiga kura kuifanya upya.
  • Wavulana wawili kutoka jamii ya wavuvi eneo la Terekeka, umbali wa takriban kilomita 75 Kaskazini mwa Juba - mji mkuu wa Sudan Kusini wanachunga mifugo hawa. Ng'ombe ni muhimu katika maisha ya jamii za watu wanaoishi Sudan Kusini
  • Hapa ni katika soko moja mjini Juba siku ya Jumatano, mfanyakazi wa Uganda anashusha kabeji zinaozingizwa nchini humo kutoka nchi jirani ya Uganda.
  • Mnamo siku ya Jumamosi wanajeshi wapya walishiriki gwaride katika kituo cha mafunzo ya kijeshi nchini Uganda.
  • Katika mji wa bandarini wa Merca, wavuvi wanakaa juu ya boti zao wakiwatupia jicho wanajeshi wa Muungano wa Afrika wakiwasili katika mji huo uliotekwa na majeshi ya AU kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabab hivi maajuzi
  • Aina ya mnyama ajulikanaye kama okapi ( dume) kutoka Kaskazini Magharibi mwa Congo, azaliwa mwishoni mwa wiki katika hifadhi ya wanyama ya Antwerp nchini Ubelgiji.
  • Hapa wenyeji wa mji wa Timbuktu nchini Mali wakusanyika kujionea viongozi wa kundi la Ansar Dine wakijiandaa kumkata mkono mtu mmoja aliyepatikana na hatia ya kuiba mchele.
  • Mwanamke mmoja akicheza densi karibu na bango kuu kuu linalotangaza tamasha la hayati Fela Anikulapo Kuti mjini Lagos, Nigeria.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.