Uchaguzi wa Marekani: Vitu 5 muhimu

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 15:53 GMT

Heka heka za uchaguzi nchini Marekani

Jumatano hii mjadala wa kwanza wa kampeini za uchaguzi wa urais nchini Marekani utafanyika .

Mwezi mmoja kabla ya siku ya uchaguzi Novemba tarehe sita, haya hapa mambo matano unayopaswa kuyafahamu kuhusu mchakato wa uchaguzi huo.

1. Kuna swala moja muhimu

Takriban asilimia 80 ya wapiga kura wanahisi kama uchumi wa nchi ni swala nyeti na mojawapo ya mambo yatakayowashawishi namna ya kupiga kura. Kulingana na utafiti uliochapishwa wiki jana na kampuni ya utafiti ya Rasmussen .

Maswala nyeti:

Uchumi
Maadili ya serikali
Kodi
Afya
Sera ya kawi
Elimu
Malipo ya uzeeni
Uhamiaji
Usalama wa kitaifa

Obama na Romney: Sera kwa sera

Swala nyeti zaidi ni uchumi na ajira kwa upande mwingine. Marais waliohudumu muhula mmoja, Jimmy Carter na George Bush Sr waliondoka katika ikulu, wakati nchi hiyo inakabiliwa na hali mbaya na kiuchumi

Ukosefu wa ajira umesalia kuwa juu kwa kiwango cha asilimia 8 kwa miezi 43 na madeni ya nchi hiyo yamepita dola trilioni 16 na hata kuwaacha watu wakijikuna vichwa kujiuliza kwa nini Rais Obama hayuko nyuma kwa kura za maoni au hata kuhoji ikiwa uchumi ni swala nyeti kwa wapiga kura kama wanavyosema wapiga kura wenyewe.

Utafiti uligundua kuwa takwimu hizi sio chanzo cha huzuni kwa wengi kama inavyodhaniwa. Waliofanya utafiti wanasema kuwa , wamarekani hawahisi kuwa wako katika hali nzuri ya kiuchumi kuliko walivyokuwa miaka minne iliyopita. Lakini hawahisi kama mambo yamewatumbukia nyongo.

Lakini kwa sababu Rais Obama havuti mkia katika kura za maoni haimaanishi kuwa swala la uchumi sio muhimu kwa wapiga kura.

Watu wengi wanahsi kuwa Rais Obama hajafanya vyema katika kura za maoni lakini pia wanahoji ikiwa Romney ataleta mabadiliko yoyote. Na pia idadi kubwa ya wamarekani wanamlaumu Rais wa zamani George W Bush kwa masaibu yao ya uchumi.

2. Ni majimbo machache tu yenye umuhimu.

Uchaguzi huu utategemea sana kura za kubahatisha au majimbo machache kwa sababu sehemu kubwa za nchi hii upande mmoja kuna wanademokrat na mwingine wanarepublican. Sidhani kama hilo litabadilika kwa hali yoyote.

Kila jimbo linapewa idadi ya wajumbe wanaoweza kupiga kura kumchagua rais kulingana na idadi ya watu katika jimbo hilo.

Uchaguzi wa Marekani 2012 takwimu na utafiti

Yeyote anaweza kushinda katika majimbo hayo.

Majimbo muhimu kumi : Florida (wajumbe 29 ), Pennsylvania (wajumbe 20), Ohio (wajumbe 18), N Carolina (wajumbe 15), Virginia (wajumbe 13), Wisconsin (wajumbe 10), Colorado (wajumbe 9), Iowa (wajumbe 6), Nevada (wajumbe 6), New Hampshire (wajumbe 4)..Pindi mgombea anapopata kura 270 unashinda urais.

Jimbo la Ohio, lina idadi kubwa ya watu wasio na ajira ikilinganishwa na idadi ya wasio na ajira kitaifa. Jimbo hilo ndio limekuwa tegemeo kubwa la wagombea kwani tangu mwaka 1960 limekuwa na usemi mkubwa nani anakuwa rais. Wagombea wote wamekuwa wakitumia mamilioni ya dola kwa kameini zao katika jimbo hili. Lina wajumbe 18 wanaoamua nani anakuwa rais.

Wenyeji wa Ohio wamekuwa wakipigiwa simu na wanaowakempenia wagombea angalau mara mbili kwa wiki katika miezi sita iliyopita. Na kila jioni matangazo ya biashara kuhusu kampeini yanaonyeshwa kwenye televisheini.

"Nimeishi katika majimbo 12 tofauti lakini sijawahi kuona matangzo ya kibiashara kuhusu kampeini za wagombea kama ya sasa kupitia redio, televisheni na nyanja mbali mbali za habari." Alisema Tim Gaddie, mwanafunzi wa chuo kikuu katika jimbo la Ohio

Ramani kuhusu uchaguzi wa Marekani

"Uchaguzi uliopita nilikuwa katika jimbo la Indiana. Kinachoudhi sana ni simu unazopigiwa lakini kinacho furahisha ni kuwa watu wamepata mwamko mpya na wanajihusisha na mjadala wa kisiasa."

Kumejitokeza taswira mbili za nchi ya Marekani wakati wa kampeini hizi, moja ambayo huwezi kukwepa matangazo mazito ya kibiashara kuhusiana na kampeini za uchaguzi, na ya pili le ambayo maisha yanaendelea tu kama kawaida kana kwamba watu hawana habari na uchaguzi.

3. Wapiga kura wanabadilika.

Kila mwezi wapiga kura wa Hispania wanaosajiliwa huongezeka hadi watu laki tano nchini Marekani. Jamii ya wahispania ilipita watu milioni hamsini mwaka 2010 ambao sasa ni asilimia kumi na tatu ya watu wote nchini humo.

Mnamo mwaka 2008, rais Obama alipokea asilimia 68 ya kura kutoka kwa walatino.Na huenda akapokea idadi hiyo mwaka huu, kulingana na mtaalamu wa siasa za Latino katika chuo kikuu cha New Mexico, Gabriel Sanchez.

Wapiga kura wanabadilika

"Hoja sio eti Romney ataweza kupokea kura za jamii ya walatino, bali ikiwa idadi ya walatino watakaojitokeza kupiga kura itamwezesha Rais Obama kushinda." Tathmini hii ni pamoja na ikizingatiwa kuwa msimamo mkali wa Romney kuhusu uhamiaji utamnyima kura za walatino.

Mwanasiasa wa Repubican Jeb Bush ametoa wito kwa Romney kulegeza msimamo huo wakati akigusia maswala yanayozua hisia kama vile uhamiahiaji hasa miongoni mwa Latino na wahispania.

Seneta Lindsey Graham amesema waziwazi kuwa idadi ya wazungu wenye ghadhabu, haijatosha kiasi cha kusalia kwenye biashara kwa muda mrefu"

4. Sio tu kuhusu Marekani

Taarifa kuhusu Iran zilizotolewa na wagombea hao wawili:

Obama: "Marekani inataka kusuluhisha mzozo huu kuhusu mradi tata wa Nuklia wa Iran kwa njia za kidiploamsia na tunaamini kuwa bado kuna muda wa kufanya hivyo, lahiki lazima tuwe na kikomo."

Romney: "Tunapaswa kuchukua hatua zozote kuilazimisha iran kusitisha mradi wake wa nuklia."

Wagombea wa uchaguzi wa Marekani Barack Obama na Mit Romney

Obama analaani siasa kali duniani.

Sera ya kimatifa inakuja ya pili katika orodha ya mambo muhimu kwa wamarekani wakati huu wa uchaguzi ingawa mauaji ya balozi wa zamani wa Libya Christopher Stevens, yameweza kuisongesha juu sera hiyo katika ajenda ya wamarekani huku Iran, Israel na Afghanistan zikijadiliwa katika vyombo mbali mbali ya habari nchini marekani.

Romney, ameshutumiwa kwa kutumia masaibu ya Libya kuhusu Marekani kushambulia sera ya Obama akisema kuwa hajakuwa mkali kwa Iran na kwamba amesaliti Israel.

Pia ameahidi kuikemea China kuhusu kile anachoita kupandisha thamani ya sarafu yake kiholela na kuhujumu thamani ya dola ya Marekani na kuongeza tisho la vuta ni kuvute ya kibiashara kati ya chi hizo.

Watu wengi wanatazama kwa karibu nani atakayeshinda uchaguzi wa marekani kwa sababu vitendo vya Marekani vina athari kubwa kwa dunia nzima.

5. Yeyote atakayeshinda, tarajia vuta ni kuvute zaidi!

Sio uchaguzi wa urais pekee utafanyika tarehe sita mwezi Novemba. Viti vyote katika bunge la waakilishi pamoja na thuluthi moja ya viti vya bunge la Senate vitawaniwa.

Wakati kinyang'anyiro cha viti hivi hakijaangaziwa sana, huenda umuhimu wake ukaathiri nafasi ya ushindi wa Rais Obama au Mit Romney.

Kibao kikielekeza wapiga kura

Chama cha Republican kinadbiti bunge la waakilishi huku Democrats wakidhibiti bunge la Senate, pande zote zimekuwa na misimamo mikali kwenye mabunge hayo, mvutano ukaendelea, na hivyo miswaada michache ikapitishwa mwaka 2011,na hivyo likaitwa bunge la kuzembea.

Dhana inayoangaziwa na kufeli kwa mwaka jana kwa kukosa kuafikia makubaliano kuhusu kumaliza madeni yanayokabili nchi hiyo, imesababisha watu kutokuwa na imani na bunge la Congress.

Lakini Rais wa zamani Bill Clinton, alielezea kuwa na matumaini kuwa anataraja bunge la congress kuwa na ushirikiano zaidi baada ya uchaguzi.

Nini maoni yako kuhusu uchaguzi unaokuja wa Marekani?

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.