Wanawake wapambe wa AVON Soweto

Imebadilishwa: 9 Oktoba, 2012 - Saa 08:27 GMT

AVON

Mwaka uliopita mauzo ya bidhaa za Avon kote duniani yalipanda kwa asili mia moja tu, lakini nchini Afrika Kusini yaliongezeka kwa karibu asilimia 30%.

Je ipi ndio siri ya mafanikio ya wanawake hawa wa Afrika kusini wanaotumia Avon?

"kila mtu anapenda Avon," Anasema Nelli Siwe, akijaribu kunishawishi kwa sauti kubwa kupita kelele za magari katikati ya mji maarufu wa Soweto, Afrika kusini.

Yeye na wenzake walianzisha kibanda cha bidhaa za urembo katika barabara yenye shughuli nyingi mjini Soweto wakitarajia kuwalenga wakaazi wa mji huo ambao ni wa kipato cha chini.

Kando yao kuna wanawake wanaochana na kurembesha nywele zao katika chumba cha ususi hafifu cha viti vya plastiki, mama akiwa amekalia uchafu huku amembeba mtoto wake mgongoni lakini akiuza mboga za spinach zilizowekwa juu ya kibao na mwanamume mwengine na miwani ya jua ambayo inauzwa kwa bei rahisi.

Wawili kati ya wanawake watano katika sayari hii wamenunua kitu kutoka Avon mwaka uliopita - na Siwe ini mmoja wa maelfu ya wanawake wanaokimbilia kuuza bidhaa hizo . Je kivutio ni nini?

Kupambana na uhalifu na kuuza mafuta ya kujipaka mwilini ni malimwengu mawili tofauti. Lakini kuuza bidhaa za Avon kulimwezesha Siwe kulipa karo ya mafunzo yake, kodi ya nyumba na gharama za usafiri. Na anasema hiyo inamuwezesha kujitegemea - hahitaji kutegemea mumewe au familia yake kupata msaada wa kifedha.

Bidhaa za Avon

"mimi ni mzee sana, natakiwa kuwa na pesa, nikiwa mwanamke haitakiwi niwaombe watu wengine pesa ," anasema Siwe.

Kwa miaka 126 tangu ilipozinduliwa huko Marekani, Avon imekuwa ikijitafutia soko kote duniani kwa ufanisi kama kampuni ya wanawake.

Nchini Afrika Kusini mfumo mbaya wa ubaguzi wa rangi na kijinsia ndio hali halisi, viwango vya ukosefu wa ajira ni vya juu sana duniani.

Mmoja kati ya watu wanne wenye umri wa kufanya kazi hawezi kupata kazi na wanawake weusi mara nyingi wako chini kiuchumi.

Hivyo basi pengine ndio sababu ya mvuto wa Avon kutoshangaza. Inawapa msimamo wa kifedha wanawake ambao hawana stakabadhi za masomo na ambao wengi wao huwa kina mama wanaojitegemea bila kupata msaada.

Avon ni maarufu kwa wateja kwa sababu wanaweza "kuinunua sasa na kulipa baadaye"

Eunice Maseko ni mzazi mmoja(hana bwana) alisoma katika Chuo kikuu cha Fort Hare Mashariki ya Cape. Ni moja kati ya taasisi kongwe ambayo kwa miaka mingi ilisaidia kujenga utawala wa watu weusi.

Kama Nelson Mandela, ambaye alifukuzwa Fort Hare kwa kujishughulisha na siasa, Maseko hakumaliza shahada yake ya degree. Juhudi zake za kupambana na ubaguzi wa rangi katika miaka ya katikati ya 80 zilisababisha masomo yake kukatizwa ghafla.

Siku moja alipokuwa akisafiri kwa "teksi" akiwa anapitia kijitabu chenye maelezo kuhusu bidhaa za AVON, msafiri mwenzake aliitisha atazame - na moja kwa moja wakaagiza na Maseko bidhaa za Avon za kiwango cha dola 80.

Avon ina sefa kedekede kwa sababu wateja wengi wanaweza kununua bidhaa hiyo na kulipa baadaye

Tukio hilo lilimpa ukakamavu wa kujihusisha kikamilifu kuuza bidhaa za Avon.

Alitupilia mbali uoga wake na akawakaribia majirani wake. Alizuru kliniki mbalimbali na maduka ya vipodozi - sehemu za umma ambazo watu wanaweza kushawishiwa kununua mafuta hayo na mengine ambayo yangemwezesha kumnunulia chakula mtoto wake wa miaka miwili.

Isitoshe watoto wake walikuwa na wajibu mkubwa mno katika siku zile za mapema.

"mvulana wangu ni mchangamfu sana na alimwambia mwalimu wake kuwa 'mamangu anauza Avon' na mwalimu akasema 'unatakiwa kuleta kitabu ili tujue anachouza'," alisema.

"alipeleka kitabu hicho shuleni na akaulizwa apeleke bidhaa hizo."

"Msichana wangu kadhalika alipeleka kitabu kwa shule - wote walijua kuwa ikiwa wangeambiwa wapeleke bidhaa hizo walikuwa na uhakika kuwa wangepata chakula baadaye siku hiyo."

"kukusanya pesa za mauzo baada ya kuuza bidhaa zangu ni kibarua kigumu. Pesa ni kidogo. Wanaagiza bidhaa matumaini yakiwepo kuwa watapata pesa za kutosha mwishoni mwa mwezi ili waweze kulipia madeni. Lakini pindi wanapopata pesa, wanakuwa na mahitaji muhimu zaidi kuliko kulipa deni la manukato kwa hivyo wanaakhirisha na kusema watakulipa mwezi ujao tena''

Hali huwa ngumu sana kwa sababu AVON haijuii mimi namuuzia nani bidhaa hizi. Wananijua tu kama mwakilishi. Kwa hivyo kama nataka sifa nzuri nitafanya kila hali kuhakikisha kuwa sifa hiyo inasalia wakati mwingine hata mimi hutumia pesa za familia kulipa madeni.

Lakini licha ya changamoto hizo, Maseko ana matumaini kuwa kuna nuru katika siku zijazo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.