Morgan Tsvangirai na jeshi la Zimbabwe

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 09:18 GMT

Waziri mkuu Morgan Tsvangirai amekuwa katika serikali ya muungano kwa miaka minne. Kulia ni waziri wa sheria Patrick Chinamasa

Wazir wa sheria wa Zimbabwe ambaye pia ni mpatanishi wa chama cha Zanu-PF Patrick Chinamasa ni wakili mmoja mrefu ambaye kwenye ukuta wa ofisi yake kuna picha za vikaragosi kuhusu mawakili walafi

Huku Zimbabwe ikijiandaa kwa mchakato wa katiba mpya pamoja na uchaguzi mpya unaonuiwa kumaliza miaka minne ya serikali ya muungano kati ya chama cha Zanu-PF na kilichokuwa chama cha upinzani, Movement for Democratic Change (MDC), bwana Chinamasa ndiye anaongoza mapatano.

Mvutano wa rasimu ya katiba unapowadia, akiwa mkuu wa kongamano la wadau na maswala nyeti kuhusu uchaguzi , bwana Chinamasa anaelezea matumaini kuhusu hatua zilizofikiwa, hatua hizo zinahusu tofauti zilizoibuka na ambazo zilisuluhishwa. Ni masawala ya sheria na swala la kutii maagizo.

Bila shaka hii inatoa picha nzuri ya nchi ambayo imepiga hatua licha ya changamoto nyingi katika miaka minne iliyopita.

Uchumi umechepuliwa , wanafunzi wanaenda shuleni, licha ya mgongano uliopo kati ya viongozi hao wawili, pamoja na maafisa wa usalama walio na mkono mkali wa sheria, viongozi wa kisiasa wa Zimbabwe wangali wanasemezana.

Lakini picha hii haijakamilika.

Mwishoni mwa mahojiano na bwana Chinamasa, nilimuuliza kuhusu swali nyeti la nini kitafanyika ikiwa kiongozi wa MDC Morgan Tsvangirai, ambaye chama chake kilishinda uchaguzi wa wabunge mwaka 2008, anaweza kushinda uchaguzi wa urais.

“Ikiwa nchi hizo za kigeni zitashawishi ushindi wa Morgan Tsvangirai, hatutakubali matokeo. Hatutakubali kabisa. Nasema kuwa hilo halitakubalika’’

''Maafisa wakuu wa jeshi tayari wamesema hadharani kuwa, hawatamkubali bwana Tsvangirai ambaye kwa sasa ni Waziri Mkuu chini ya serikali ya muungano kuwaongoza. Swala hilo hata hivyo ataweza kulijibu vipi bwana Chinamasa ambaye pia ataelezea ikiwa huo ndio msimamo rasmi wa chama cha Zanu PF?

''Hapa ineonekana unataka mashaka'' alisema bwana Chinamasa

Alifafanua alichokuwa anamaanisha

“Tsvangirai hawezi kushinda. Amekuwa akifanya kampeini na kutaka uungwaji mkono dhidi ya maslahi ya wazimbabwe hasa kuhusu maswala mengi, mfano maswala kama ardhi na kutaka kuhujumu maendeleo na hatua ziliziofikiwa tangu uhuru.

"Na hapa sasa ndipo jeshi linaingia , vijana walihusika katika harakati za uhuru ili kudhibiti maslahi yetu. Marafiki wengi walifariki, na wamezikwa katika makaburi yasiyojulikana. Jeshi la Zimbabwe halimtaki Morgan Tsvangirai kuliongoza.”

"Na sasa ikiwa mtu atasema kuwa ,wakati nitakapoingia mamlakani, nitabadilisha hilo, jeshi lina haki ya kusema, tafadhali hivi unatafuta matatizo. Tsvangirai atakuwa anatafuta matatizo kutaka kubadili sera ya ardhi. Hakuna mtu yeyote atakubali utumwa'' alisema kwa ukali bwana Chinamasa

Nilimtaka afananue anachomaanisha anaposema Tsvangirai atakuwa anatafuta matatizo na akasisitiza kuwa hatakubali kabisa urais wa Tsvangrai kwa hali yoyote

Jeshi la Zimbabwe

Alisema "unaweza kutafsiri matamshi yangu unavyotaka.’’

Lakini ninapomuuliza yeye kunipa tafsiri yake, Chinamasa alisema kuwa “ Najua Tsavangirai ni kipenzi cha nchi ambazo ziko katika msitari wa mbele kuziwekea nchi zingine vikwazo.Na ikiwa nchi hizi zitataka Tasvangiraui ashinde kwa lazima, hatutakubali matokeo ya uchaguzi huo. Hatutakubali. Yaani hatutakubali kabisa matokeo kama hayo. Je hilo halieleweki?" alihoji bwana chinamasa

Haya mambo ndio hayo.

Bwana Tsvangirai akishinda – sisemi kama ni wazi Tsvangirai atashinda, na ikiwa Zanu-PF itadai kuwa ameshinda kwa sababu ya kuungwa mkono na chi za kigeni , bwana Chinamasa anasema hatakubali kamwe matokeo hayo.

Je unadhani kama hii ni sawa? Na unayatafsiri vipi matamshi ya bwana Chinamasa kuhusu uchaguzi huru kufanyika nchini Zimbabwe mwaka ujao?

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.