Kipindi kilichopita: Kaunti ya Kisumu

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 13:42 GMT

Washiriki wa kipindi cha Sema Kenya.

Jumapili iliyopita kipindi cha Sema Kenya kilikuwa katika Kaunti ya Kisumu kuangazia maswala ya mkoa wa Nyanza.

Mji wa Kisumu ndio makao makuu ya Kaunti hii, na pia ndio mji wa nne kwa kubwa, kwa idadi ya watu, baada ya miji za Nairobi, Mombasa na Nakuru.

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Kisumu ilikuwa ni mojawapo ya maeneo yaliyokumbwa na vurugu na uharibifu mkubwa wa mali na biashara.

Inadaiwa pia kwamba wengi walioshiriki katika maandamano yaliyokuwemo ya kupinga matokeo ya uchaguzi, yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi, waliuawawa kwa kupigwa risasi.

Kaunti ya Kisumu ina maeneo bunge sita; Nyakach, Nyando, Muhoroni, Kisumu Mashariki, Kisumu Magharibi na Kisumu vijijini.

Eneo hili ni ngome ya chama cha ODM ambacho kinaongozwa na Waziri Mkuu Wa Kenya, Raila Odinga. Maeneo bunge yote sita yanawakilishwa na wabunge wa chama cha hicho cha ODM.

Ilhali maeneo bunge ya Kisumu Mashariki na Magharibi wamechanganyika kutoka jamii mbalimbali, maeneo hayo mengine yana kaliwa na jamii ya kiasili ya wa Luo.

Baadhi ya shughuli za biashara zinazoendelea katika eneo hili ni pamoja na uvuvi na upanzi wa miwa na mchele.

Kwa upande wa kilimo, kaunti hii inaongoza kwa viwanda vya kuzalisha sukari vya Kibos, Miwani, Chemilil. Bali na uzalishaji wa Sukari, wakaazi wa kaunti hii pia wana kuza mchele kwa wingi katika maeneo ya Ahero na Kabonyo.

Hata hivyo, wakaazi wengi wa Kaunti hii wanakabiliwa na umaskini mkubwa huku idadi kubwa ya raia wakiwa hawana ajira.

Japo Kaunti hii ya Kisumu inapakana na Ziwa Victoria, ambayo ndiyo kubwa zaidi barani Afrika, inakabiliwa na uhaba wa maji safi.

Tatizo lingine ni gugu maji kwenye Ziwa ambalo linaathiri shughuli za uvuvi na uchukuzi wa bidhaa.

Ingawa kinara wa chama cha ODM, Raila Odinga, ana ushawishi mkubwa kisiasa katika eneo hili, mchakato wa kupata wagombea katika nyadhifa za uongozi katika chama hicho unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, ikikumbukwa kwamba ni wabunge wachache tu wamewahi kurudi bungeni baada ya msimu wao wa kwanza.

Kipindi hicho pia kiliweza kusikika kwenye redio kupitia Idhaa ya Dunia ya BBC (Nairobi, Mombasa 93.9FM, Kisumu 88.9FM) na pia kwenye redio ya Pamoja (99.9FM Nairobi) hapo Jumapili saa saba alasiri.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.