Barack Obama, je alikuwa mwokozi?

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 08:47 GMT

Obama alikosea wapi?

Barack Obama aliapishwa kama rais wa Marekani kwa kauli mbiu ya ‘MATUMAINI’ lakini miaka minne baadaye Obama ambaye ni bingwa wa kusema na ambaye aliingia mamlakani kwa kuwapa watu matumaini , anaonekana amegeuka na kuwa mtu ambaye aliyenaswa na hali ngumu kulingana na mwandishi maarufu Andrew Marr

Nani ambaye angedhani hali hii ingejitokeza kwa Obama?

Nani – wa mrengi wa kulia au kushoto, wa Democrat au wa Republican ambaye angeamini miaka minne iliyopita kuwa Barack Obama atakabiliwa na kibarua kigumu kisiasa?

Huyu alikuwa mtu ambaye alifananishwa wakati mmoja na mtabiri wa kisiasa, mwokozi , mponyaji ambaye angewaunganisha wamarekani na kuondoa kabisa hali ya ghadhabu kuhusu uliokuwa uongozi wa rais Mustaafu George Bush

Na sasa anakaribia kushindwa na mgombea wa upinzani ambaye ni tajiri kupindukia, ambaye naye wafuasi wake hivi karbuni waliondokewa na matumaini naye Mit Romney.

Watu kadhaa waliohojiwa katika miji ya Chicago, Washington na New York swali moja rahisi sana la, 'Je matumaini yalienda wapi?'

Rais Barack Obama

Je ni mdororo wa mwaka 2008 na tisho la mdororo mbaya sana ambao ulifuta matumaini ya watu?

Je zilikuwa ahadi zake ambazo hangeweza kuzitimiza pamoja ya kukosa uzoefu? Je ilikuwa mfumo mbaya wa siasa za Marekani au tu kwamba watu hawampendi tena?

Bila shaka kulikuwa na uelewa kuhusu changamoto za kiuchumi ambazo zilimkabili Rais Obama kabla hata ya kuapishwa kwake kama rais.

Wengi walihisi kuwa mfumo wa kibepari wa nchi hiyo ulikuwa unakaribia kutumbukia nyongo.

Obama aliuchepu uchumi wa marekani na kuukoa kutokana na kuporomoka na kisha akaokoa sekta ya viwanda hususan uundaji wa magari

Ishara ya mabadiliko na wakala wa mabadiliko ni vitu viwili tofauti.

Lakini wachumi wengine walihisi kuwa alikosea , kwa kutochukua nafasi ya kubadili mfumo mzima

Jeffrey Sachs, mwanauchumi mashuhuri duninai anasema kuwa kuongeza dola trilioni moja kwa hazina ambayo tayari inakabiliwa na madeni ni kitu cha kushangaza.

Anahisi kuwa serikali ya Obama ilikuwa haikkabiliani na tatizo la uchumi ambao hauna usawa na ambao haukan uekezaji mkubwa na ambao tayari ulisababisha watu nchini humo kutafura ajira kwingineko duniani.

Obama hapa akifanya mazoezi

"Hali ya nchi hii si nzuri. Tuna asilimia kumi na tano ya watu wanosihi katika umaskini na tuna kila mu mmoja katika watu saba anayetegemea chakula cha msaada , watu wetu wengi wanakaribiwa kutumbukia katika umaskini kumaanisha kuwa ni watu wengi sana wanakabiliwa na wakati mgumu kiuchumi.’’

Bila shaka ni matatizo haya ambayo yamewafanya wengi kususia Obama na hivyo kuifanya kampeini ya Romney kuwa na ushawishi.

Mpango wa afya wenye mageuzi makubwa na ambao Obama alijaribu sana kushawishi ili uungwe mkono ndio mojawapo ya mambo yaliyomletea masaibu anayokabiliwa nayo sasa hivi katika kura za maoni.

Mpango huo ambao ulipingwa na wengi ulikiletea chama cha Democrat matokeo mabaya sana kuwahi kuonekana tangu mwaka 1948 na hivyo kupunguza ushawishi wa Obama .

Obama alinena ‘ NDIO TUNAWEZA,’ lakini ameshindwa kufanya kwa vitendo.

Kuhusu sera ya kigeni kuuwawa kwa Osama Bin Laden, na kutumia ndege zisizo na rubani kushambulia Taleban nchini Pakistan, imeungwa mkono sana

Lakini ahadi za Obama kufunga kambi ya Guantanamo Bay na kuleta uaminifu kati ya waisilamu na wamarekani, bado hazijatimizwa. Inaoenekana Obama aliahidi mambo mengi kuliko uwezo wake wa kuyatimiza.

Ni kweli kwamba katika bunge la Congress , wabunge wa Republican walifanya kila hali kumtatiza Obama na kufanya mambo kuwa magumu kwake.

Ukosoaji mkubwa na kejeli alizofanyiwa Rais Obama na wanaharakati wa chama cha Tea Party zilikuwa mbaya mno. Lakini yote Obama aliyachukua kwa moyo mmoja.

Rais Obama akiwa kazini mjini Washington

Hata hivyo Obama lazima akubali mapungufu yake katika kuwasilisiliana na watu.

Mwandishi wake, Jodi Kantor, anasema kuwa Obama hutegemea sana mawazo yake katika kufanya uamuzi.

Na sasa kama rais mstaafu, Bill Clinton amekuwa akitoa matamshi yenye uzito na ambayo yanalenga kumsaidia Obama katika kampeini yake kabla ya uchaguzi mkuu siku ya Jumanne mpaka Obama akawa anamuita waziri wake wa mambo ya kigeni katika kuweka wazi mambo.

Wakati huohuo wamarekani wao wanaonekana kuishi katika dunia yao aidha akiwa wa democrat au Republican wakisikiliza vyombo tofauti vya habari kuhusu maoni ya watu wala hawazungumzi miongoni mwao.

Obama bila shaka ni mtu mwenye akili nyingi na anayeoendwa na watu. Lakini yeye sio mwokozi ambaye wamarekani wengi walimdhania kuwa walipompigia kura kwa wingi miaka minne iliyopita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.