Sema Kenya Nyeri

Imebadilishwa: 22 Novemba, 2012 - Saa 12:55 GMT

Washiriki wa kipindi cha Sema Kenya Makueni

Kaunti ya Nyeri ilijulikana sana kwa kuwa makao makuu ya uliokuwa Mkoa wa Kati kabla ya mikoa kufutiliwa mbali na katiba mpya ya Kenya ya mwaka 2010.

Nyeri pia inasifika kwa watu mashuhuri wanaotoka huko akiwemo Rais wa Jamhuri ya Kenya Mwai Kibaki, mshindi wa tuzo la Nobel Profesa Wangari Maathai, shujaa wa kupigania uhuru Dedan Kimathi na wengineo.
Nyeri inajumuisha maeneo bunge sita; Nyeri mjini, Mukurweini, Othaya, Mathioya, Kieni na Tetu.


Idadi kubwa ya wakazi wa Nyeri ni jamii ya WaKikuyu ingawa kuna watu kutoka jamii nyingine kama vile WaMeru, WaKamba, WaHindi, WaMaasai na WaSomali.


Uchumi wa Nyeri hutegemea pakubwa ukulima haswa majani chai na kahawa.
Wiki hii, wakazi wa Kaunti ya Nyeri wapatao 100 na jopo la viongozi watakutana kuyajadili masuala yanayohusu eneo hilo katika kipindi cha Sema Kenya.


Baadhi ya masuala yaliyozungumziwa katika kikao hicho, ni ulevi na uuzaji wa pombe haramu, ukosefu wa usalama, ukosefu wa ajira na kuwepo kwa makundi haramu. Eneo za Mukuruweini na Mathira zinakabiliana na shida ya kunyanyaswa na kundi haramu la Mungiki. Kundi hilo kawaida hudai asilimia 10 ya mauzo ya wanabiashara.


Kiwango cha elimu pia kimeathirika sana Nyeri huku vijana wengi wakiachia masomo yao wakiwa katika shule za msingi licha ya kuwa na shule nyingi za sekondari zenye umaarufu sana kama vile Nyeri, Kagumo na Ngandu.
Ulevi na utumizi wa madawa ya kulevya pia unasemekana kuiathiri jinsia ya kiume eneo hili.
Haya yote yamechangia kuzorota kwa uchumi wa Kaunti ya Nyeri.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.