Sema Kenya kipindi cha Trans Nzoia

Imebadilishwa: 6 Disemba, 2012 - Saa 15:10 GMT

Wakazi wa Trans Nzoia wakiwa katika kipindi cha Sema Kenya.

Sema Kenya ilizuru Kaunti ya Trans Nzoia. Kaunti hii ina maeneo bunge tano yakiwa ni: Kwanza, Cherangany, Endebess, Kiminini na Saboti.

Ingawa kaunti hii hukuza mahindi kwa wingi, wakulima wa Trans Nzoia wanakabiliana na matatizo mengi. Kaunti hii haina viwanda vya kukausha mahindi hivyo kuwalazimisha wakulima kusafirisha mazao yao nje ya kaunti kutafuta huduma hiyo.

Eneo hili pia halina kiwanda cha kusaga unga. Wanapowasilisha mahindi yao kwenye bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao (NCPB), wakulima wanasema hawapati bei bora.

Changamoto ingine wanayokabiliana nayo wakulima ni bei ghali ya mbolea. Wanalalamika kuwa mbolea inayofaa kutoka kwa bodi kwa bei nafuu hucheleweshwa hivyo kuwalazimisha kununua ile inayouzwa na makampuni ya kibinafsi kwa bei ya juu.

Hoja ingine wanayo wakazi wa Trans Nzoia ni hali duni ya miundombinu hasa barabara za kusafirishia mazao yao. Hizi zinasemekana kuwa katika hali duni hapa ikikumbukwa kwamba kaunti haina viwanda vya kusaga mahindi na kwa hivyo inabidi mazao yasafirishwe nje ya kaunti.

Bali na hayo, kuna ukosefu wa usalama katika baadhi ya sehemu za kaunti hii hasa mjini Kitale na mipakani mwa kaunti hiyo na eneo la Pokot Magharibi na Mlima Elgon.

Ugavi wa ardhi na shida ya wakimbizi wa ndani kwa ndani pia ipo na inafaa kutatuliwa.

Haya ndio yaliyozungmziwa katika kipindi chetu cha Sema Kenya mjini Kitale kati ya wakazi wa Kaunti ya Trans Nzoia na viongozi wao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.