Je Zuma atahimili mawimbi ya ANC?

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 12:08 GMT

Jacob Zuma na makamu wake anayetarajiwa kugombea uongozi wa chama dhidi yake, Kgalema Motlanthe

Chama tawala nchini Afrika Kusini kinajiandaa kwa mpambano wa uongozi wa chama ambao utaamua ikiwa utaendeleza kile ambacho wengi wanatafsiri kama ukosefu wa kuondokana na madhambi ya enzi ya ubaguzi wa rangi.

Au ikiwa itakuwa fursa ya kuondokana na historia ya nchi na kuipa nchi hiyo ambayo ina uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, mustakabali mwema

Hapa kinyan'anyiro huenda kikawa kikali kwa Rais Jacob zuma. Anatarajiwa kugombea muhula mwingine kama kiongozi wa chama katika eneo la Mangaung, ambako chama cha ANC kilizinduliwa karne moja iliyopita.ANC ikiwa na wingi wa wafuasi, yeyote atayeshinda uongozi wa chama, bila shaka atashinda katika uchaguzi wa urais utakaofanyika baadaye mwaka 2014.

Mwaka 2007, rais Zuma alisaidiwa kushinda uchaguzi wa urais katika kongamano kama hili linalotarajiwa mjini Polokwane, wakati alipomshinda aliyekuwa rais Thabo Mbeki.

Tangu chama cha ANC kuanza kupokea uteuzi wa wagombea tarehe mosi Oktoba, wale wanaomuunga mkono Zuma kuongoza kwa muhula wa pili, wanaonekana kuwa wengi ikilinganishwa na wale wanaomuunga mkono naibu wa Zuma, Kgalema Motlanthe - ambaye ndiye mgombea mwingine pekee.

Mafanikio ya Rais Zuma katika muhula wake wa kwanza kama rais, yameonekana kuathirika kutokana na mauaji ya Marikana ambako wachimba migodi 34 waliokuwa wanagoma waliuawa na polisi.Ilikuwa wakati wa mgogoro kuhusu mishahara ya wachimba migodi hao katika mgodi wa lonmin. Wakosoaji wake wanasema mtindo wa uongozi wa Zuma ambao ni wa kujivuta, unachochea kudorora kwa uchumi pamoja na kukidhoofisha chama cha ANC.

Kashfa nyingine ambayo inamkuba Zuma ambaye wakati mwingine anajulikana kama Msholozi, ni madai ya kutumia vibaya mali ya umma kukarabti nyumba yake kijiji kwao Nkandla.

Mdhibiti wa mali ya umma anachunguza ikiwa idara ya serikali inafadhili ukarabati huo, wakati huu ambapo wachimba migodi wanalipwa pesa kidogo sana.

Wengi wanahofia ikiwa sifa ya rais mustaafu Nelson Mandela itasalia kudumu

Bwana zuma amekana kukiuka sheria akisema kuwa aliomba mkopo wa kufanya ukarabati huo.
Kashfa nyingine inayomzonga Zuma ni ile ya ufisadi. Kuna madai kuwa chini ya utawala wake , ufisadi umekita mizizi na kwamba familia yake inanufaika na mapendeleo kwa kupata mikataba ya kibiashara kwa sababu ya kutoka kwa familia ya uhusiano wao.

Kikulacho ki nguoni mwako.

Mwandani wake ambaye sasa ni hasimu wake wa kisiasa,bwana Mbeki alivunja kimya chake cha miaka minne alipoanza kumshambulia Zuma kwa uongozi akisema kuwa ana wasiwasi kuwa Afrika Kusini inakosa mwelekeo na kwamba wananchi wanakubali kuongozwa kwa njia isiyo faa na ambayo baadaye itasababisha mzozo mkubwa.

Bwana Mbeki alisema "kwanza sielewi ambako nchi hii inaelekea. Na sijui hatua ambazo naweza kuchukua kukabiliana na kitu ambacho kinatishia nchi hii hasa nchi kukosa mwelekeo wa uongozi"

Changamoto kubwa kwa zuma hatioki kwa upinzani bali kwa chama chake.

Bwana Motlanthe, 63, ni mwanasiasa mwenye kusifika kwa kuwa alikuwa mfungwa wa zamani wa kisiasa, lakini haonekani kama anataka sana kuwania urais. Alihudumu kama rais wa nchi hiyo kwa miezi sita baada ya aliyekuwa rais Thabo Mbeki kuondoka mamlakani.

Akilinganishwa na Zuma bwana Motlanthe hana sifa kama za Zuma, yeye ni mtu ambaye hapendi kujionyesha kwa umma sana. Ni msiri na mtulivu sana

Ameteuliwa kuwania urais na jimbo lenye utajiri mkubwa zaidi Afrika Kusini la Gauteng wakati majimbo sita kati ya tisa yanamuunga mkono bwana Zuma.

Anasema ana wakati mgumu kutafakari ikiwa atamenyana na Zuma kuwania urais.

Kgalema Motlanthe

Bwana Motlanthe anaungwa mkono na Julius Malema, ingawa amepuuza uungwaji huo akisema vijana wa ANC hawana kura nyingi katika kongamano la chama. Bwana Motlanthe hataki kutaifishwa kwa migodi ya Afrika Kusini kinyume na anavyotaka Bwana Malema.

Ikiwa atagombea urais dhidi ya Zuma, huenda akapatia chama cha ANC uhai , lakini akishindwa basi ndio itakuwa mwisho wa maisha yake katika chama cha ANC Kwa nini bwana Zuma angali anapendwa na wengi?

Mwisho wa fungate

Zuma amefanikisha vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya HIV

Zuma anapendwa na wengi, na chini ya uongozi wake, juhudi dhidi ya virusi vya HIV zinasemekana kuzaa matunda Pia nchi yake iko chini ya muungano wa nchi zinazokuwa kwa kasi zaidi pamoja na hayo mwenyekiti mpya wa muungano wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye ni mke wa zamani wa Zuma, alichaguliwa kama mwenyekiti mpya wa Muungano wa Afrika.

Wengi katika ANC wanaamini kuwa ikiwa Zuma ataongoza nchi kwa muhula mwingine, itakuwa nduio mwanzi wa mwisho wa chama cha ANC

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.