Je raia wa Afrika Kusini wanashangazwa na ubakaji?

Imebadilishwa: 10 Januari, 2013 - Saa 17:14 GMT

Msichana mmoja alibakwa katika eneo hilo tarehe 2 Januari

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa bado anaishi katika chumba kimoja katika mtaa wa mabanda wa Soweti wakati polisi walipokuja kumkamata siku chache kabla ya mkesha wa siku kuu ya mwaka mpya.

Kwa mujibu wa mashahidi kadhaa, mtu huyo alikuwa amembaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na saba katika baa moja, na alihisi kuwa kitendo hicho ni cha kawaida na hivyo hakujaribu kutoroka.

Hamna hata mtu mmoja katika baa hiyo, mbali na msichana huyo alifikiria kupasha polisi habari kuhusiana na tukio hilo.

Wakati ambapo taifa la India, linachunguza sheria za nchi hiyo kufuatia tukio la ubakaji, Afrika Kusini inaonekana kuwa imezembea.

Serikali ya nchi hiyo imeonekana kutojali yale yanayotendeka licha ya takwimu kubainisha viwango vya ubakaji nchini humo viko juu hata kuliko taifa la India.

Vijana katika eneo la Soweto

Visa elfu sitini vya ubakaji huripotiwa kila mwaka nchini Afrika Kusini, idadi ambayo ni maradufu ya visa vinavyoripotiwa nchini India.

Lakini wataalamu wanahisi kuwa visa hivyo huenda vikawa vingi zaidi kwa kuwa mara nyingi wasichana wanaobakwa huwa hwajitokezi kutoa habari kwa polisi.

Mapema wiki hii vyombo vya haabri nchini Afrika Kusini, vilichapisha habari kuhusu kile kinachosemekana kuwa mtindo mpya, ambao wanawake wakongwe ndio wanaolengwa na wabakaji.

Nyingi ya visa hivyo hulenga kina mama walio na umri mkubwa katika maeneo mashambani.

Katika matukio haya wamama wawili walio na umri wa miaka 82 na 73 walibakwa tarehe mbili mwezi huu.

Licha ya hasira na ghadhabu iliyojitokeza miongoni mwa raia wa nchi hiyo ambao walipiga simu katika vituo vya radio, viongozi wa taifa hilo bado hawajaona umuhimu wa kukabiliana na janaga hilo.

Katika siku za hivi karibu, waandishi wa habari na wanaharakati wa kijamii, wamekuwa wakichunguza matukio yanayoendelea nchini India, huku wakiwa na matumaini kuwa yangelitendeka nchini humo, kwa kuwa kujadili suala hilo pekee halitoshi.

Kuna idadi kubwa ya wabakaji Afrika Kusini

Mpumelelo Mkhabela Mhariri wa gazeti moja la Soweto

Mhariri mkuu wa gazeti la Mpumelelo Mkhabela, la Soweto, Mpumelelo Mkhabela, amesema kuna haki ya raia wa nchi hiyo kujitokeza zaidi na kupambana na tatizo la ubakaji.

Mkhabela, kwa upande mmoja anasema serikali ya nchi hiyo imejitahidi, lakini raia nao wanapaswa kujitolea na kuchangia katika harakati hizo, badala ya kuonyesha ghadhabu kwa siku moja.

Kwa sasa inakisiwa kuwa Afrika Kusini, ndilo taifa linaloongozwa kwa visa vya ghasia na ubakaji barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Visa vya ubakaji vimekuwa vikiendelea kwa kwa miongo kadhaa na raia wengi wanayaona kama ni matukio ya kawaida.

Katika jamii nyingi nchini humo, kina mama huzungumzia jinsi wanavyotarajia kudhalalishwa huku wavulana nao wakiishi huku wakiwa na dhana kuwa wao wana haki zaidi kuliko wasichana na kina mama.

Lakini mapema wiki hii, raia wa nchi hiyo walighadhabishwa sana na tukio la kubakwa kwa msichana mmoja, mwenye umri wa miaka 21, na kundi moja la vijana, tukio ambao ambalo limeangaziwa pakubwa na vyombo vya habari nchini humo.

Wasichana na wamama wanaishi kwa wasiwasi

Msichana mmoja katika mtaa wa Soweto

Msichana huyo alibakwa akiwa njiani kwenda kujisajili katika chuo kimoja kikuu nje ya mji wa Pretoria.

'' Kwa sasa hatuko salama hata kidogo, kila siku tunahofia kuwa unaweza kubakwa'' Alisema msichana mmoja katika chuo hicho.

Ripoti zinasema msichana huyo alikamatwa na watu wanne ambao walimvuta hadi kichakani ambako walianza kumbaka.

Kwa bahati nzuri msichana huyo alinusurika.

Wanafunzi wengi katika chuo hicho ambao hawakuwa wamesikia tukio hilo, hawakushangzwa.

Wengi wao walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kupiga foleni ili kutafuta nafasi ya kusoma licha ya jua kali..

Mwanamme mmoja ambaye alikuwa akipita hapo alikiri kuwa kuna idadi kubwa ya wabakaji katika eneo hilo.

Kwa mshangao mama mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakipiga foleni, aligeuka huku akiwa na hasira, na kusema '' Sijui ni nini mbaya na wanaume wa siku hizi''.

'' Ni lazima jambo la dharuru lifanyike ili kukabiliana na matukio ya ubakaji'' alisema msichana huyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.