Kaunti ya Isiolo

Imebadilishwa: 10 Januari, 2013 - Saa 14:31 GMT

Washiriki wa kipindi cha Sema Kenya

Sema Kenya ilitembelea Kaunti ya Isiolo kuendeleza mazungumzo ya kitaifa kwa kuwajumuisha wakazi wa eneo hilo na viongozi wao.

Hadi sasa, Sema Kenya imeweza kuzuru eneo mbalimbali za taifa kama vile Mombasa, Kisumu, Kajiado, Nyeri, Makueni, Kitale na Nairobi.

Kama ulivyo mtindo, kipindi hiki kikiwa Isiolo kiliwaleta wakazi 100 na jopo la viongozi wanne kuyajadili masuala yanayohusu kaunti hiyo.

Mji wa Isiolo ulikuwa karibu na kambi za wanajeshi wakati wa ukoloni. Wanajeshi walipostaafu, wengi wao wakiwa wa jamii ya WaSomali, walifanya makazi yao hapa. Kisha jamii mbalimbali kama vile WaBorana na WaMeru ziliwasili na kutua huko.

Isiolo inashirikisha maeneo bunge ya Isiolo Kaskazini na Isiolo Kusini. Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, idadi ya watu wanaoishi katika kaunti hii ni 143,000.

Mji wa Isiolo ulitengwa kutoka wilaya ya Nyambene na kuteuliwa kuwa makao makuu ya wilaya ya Isiolo.

Jamii za WaSomali, WaRendille, WaTurkana, WaSomali na WaBorana zinapatikana katika mji huo.

Baadhi ya masuala yaliyozungumziwa katika mjadala wa wiki hii ni ukosefu wa usalama na wizi wa mifugo, kuathirika kwa sekta za mifugo kama vile ufugaji wa ngamia na mbuzi, umiliki wa ardhi na mengineo.

Waziri wa maendeleo ya kasakazini ya Kenya Mohammed Elmi, Kamishna wa Kaunti ya Isiolo Wanyama Musiomba, wagombea vyeo na maafisa wa serikali na mashirika ya kijamii walikuwa katika jopo letu kujaribu kuzitatua hoja za wakazi wa Isiolo.

Ilibainika kwamba ukosefu wa usalama umeiathiri Kaunti ya Isiolo pakubwa na kuzorotesha uchumi wa eneo hilo. Kwa mfano mkazi mmoja alisema ufugaji wa ngamia ulikuwa unailetea kaunti shilingi milion 1.2 kila mwezi na sasa hiyo biashara imekoma.

Bei ya maziwa nayo ilisemekana kwenda juu sana kiasi kwamba chupa iliyokuwa inauzwa shilingi 17 sasa inauzwa shilingi 60.

Wakazi walitaka serikali idumishe usalama ili uchumi uweze kuinuka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.