Sema Kenya Mji wa Eldoret

Image caption Washiriki wa kipindi cha Bungoma

Wiki hii SemaKenyaitakuwa mjini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu.

Eneo hili lilishuhudia machafuko mabaya zaidi ya kisiasa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Miaka mitano baadaye Kaunti ya Uasin Gishu inashiriki tena uchaguzi mkuu hapo Machi nne.

Licha ya juhudi za kurejesha amani, kungali na wakimbizi wa ndani katika eneo hili. Taswira hii inazua hoja ikiwa majaaliwa ya maridhiano baina ya jamii zinazoishi Uasin Gishu yameafikiwa.

Mji wa Eldoret ndio makao makuu ya Kaunti ya Uasin Gishu ambapo pia kuna maeneo bunge sita ikiwa ni pamoja na Ainabkoi, Turbo, Kapseret, Moiben, Soy na Kesses.

Uasin Gishu ndio kitovu cha sifa ya Kenya katika ulingo wa riadha ambapo wametoka mabingwa wa kimataifa akiwemo mwanariadha wa miaka ya hamisni Kipchoge Keino, wengine ni Moses Kiptanui na Ezekiel Kemboi.

Kilimo ndicho kinachotegemewa zaidi kuleta mapato kwa wakaazi wa eneo hili ambapo wanazalisha nafaka kwa wingi. Sekta ya viwanda imeanza kupanuka.

Katika ustawi wa miundomsingi, Uasin Gishu inajivunia kua na uwanja wa kimataifa wa ndege. Barabara kuu inayounganisha Afrika Mashariki imepitia mji wa Eldoret, bomba la mafuta na reli. Sekta ya afya imefanikishwa na Hospitali ya pili ya kitaifa na Chuo Kikuu cha Moi.

Jukwaa la Wakenya kupitia makala ya SemaKenyalinapambwa na wakaazi wa Kaunti ya Uasin Gishu na watakua na nafasi ya kuwahoji viongozi wao.

Ukiwa NchiniKenyajiunge na mjadala huu katika runinga ya KTN jumapili 12 jioni. Pia mjadala unaletwa kwako na Idhaa ya Kiswahili ya BBC (Nairobi,Mombasa93.9FM, Kisumu 88.1FM) saa Saba Adhuhuri saa za Afrika Mashariki.