Kuhusu uchaguzi wa Kenya

Wapiga kura nchini Kenya, watamchagua rais mpya tarehe 4 mwezi Machi ukiwa ni uchaguzi wa kwanza tangu uchaguzi wa Disemba mwaka 2007/2008 ambapo ghasia zilizuka baada ya kuibuka utata. Zaidi ya watu elfu moja waliuawa na sifa ya nchi ikaharibika sana.

Wakati wa uchaguzi huu wakenya watawachagua rais, wabunge na maseneta, magavana na viongozi wa kaunti.

Rais Kibaki hagombei tena muhula mwingine. Bali Waziri mkuu Raila odinga na mwenzake katika serikali ya Muungano iliyokumbwa na misukosuko.

Wadhifa wa waziri mkuu uliundwa wakati wa mazungumzo ya amani yaliyosimamiwa na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan, utasita kuwepo wiki ijayo.

Lakini bado kuna mengi ya kuzungumziwa kabla na baada aya uchaguzi. Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta pamoja na mgombea mwenza William Ruto wanakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita katika ICC na punde baada ya uchaguzi hawatakuwa na budi ila kwenda huko.

Ruto ambaye watu wa jamii yake ya Wakalenjin na ile ya Uhuru ya wakikuyu, wameungana na Kenyatta kuunda serikali ya muungano . Jamii hizi mbili ndizo zilipigana sana. Wameungana kugombea chini ya muungano wa Jubilee dhidi ya Raila Odinga.

1. Je kesi za ICC dhidi ya Uhuru na Ruto zimeathriri kampeini za uchaguzi?

Kesi inayokuja dhidi ya wawili hao, ndilo swala limejadiliwa sana kuliko hata wagombea wanavyouza sera zao, kuhusu ukosefu wa ajira, miundo msingi, huduma za kijamii na hata swala la Tisho la ugaidi kutoka kwa nchi jirani ya Somalia.

Image caption Uhuru Kenyatta na William Ruto

Swala hili limeigawanya nchi na kuonyesha ukabila zaidi, kunao wanaiokosoa mahakama hiyo hasa watu wa makabila ya Kikuyu na Kalenjin

Kenyatta anatoka katika kabila la Kikuyu wakati Ruto anatoka jamii ya Kalenjin.

Kesi hii imeonyesha sana ambavyo nchi za Magharibi zina wasiwasi ikiwa Kenyatta na Uhuru watashinda uchaguzi huu.

Badala yake wanaishutumu mahakama hiyo kwa kujaribu kuwashawishi wakenya nani wampigie kura.

Ubalozi wa Uingereza nchini humo, ulisema hautamuunga mkono mgombea yeyote lakini serikali yoyote itakayoingia mamlakani lazima iwe tayari kushirikiana na mahakama hiyo

Mabalozi wengine wamesema kuwa hawatajihusisha sana na watuhumiwa wa ICC ikiwa watashinda uchaguzi

Uhuru Kenyatta na William Ruto wanajiwakilisha kama waathiriwa wa njama ya nchi za Magharibi na kusema kuwa Odinga ni kibaraka wan chi hizo na mtu aliyewaletea masaibu yao.

2.Je kuna uwezekano wa ghasia kutokea tena?

Wagombea wa uchaguzi wameahidi kukubali kushindwa ikiwa watashindwa. Serikali imepiga hatua kudhibiti matamshi ya uchochezi au chuki kuenezwa. Idara ya polisi imepanuliwa kuweza kudhibiti maneno ambayo huenda yakakumbwa na ghasia, huku asasi za kijamii nazo zikifanya kampeini kali kuhamasisha jamii dhidi ya kujihusisha na ghasia.

Rais Barack Obama aliwahutubia wakenya kwa njia ya video akisema uchaguzi huu unatoa fursa kwa wakenya kutangamana badala ya kuvurugana.

Hata hivyo, kwa sasa kuna wasiwasi kwa sababu kuu ya ghasia zilizotokea ambayo ilikuwa ukabila bado haijaweza kushughulikiwa.

Shirika la Human Rights Watch, lilionya kuwa sababu zilizosababisha ghasia baada ya uchaguzi zingali kutatuliwa.

3. Je mfumo utafanya vipi kazi?

Kufuatia mabadiliko katika mfumo wa kisiasa, Kenya itafanya uchaguzi wake wa kwanaza ambapo watawachagua zaidi ya wajumbe watatu. Wagombea wa urais lazima wawe wakenya na wala wasiwe na uraia mwingine wa kigeni.

Mshindi lazima apate zaidi ya asilimia hamsini ya kura katika duru ya kwanza na takriban asilimia 25 katika nusu ya majimbo 47 kote nchini.

Ikiwa hakuna mshindi katika duru ya kwanza , duru ya pili itafanyika terehe 11 Aprili.

Matokeo rasmi ya duru ya kwanza yatatangazwa tarehe 11 Machi. Rais mpya ataapishwa tahere 26 Machi.

Wapiga kura lazima wawe na zaidi ya miaka 18

Takriban watu milioni 14.3 wamesajiliwa kama wapiga kura

4.Wagombea wakuu ni akina nani?

http://www.bbc.co.uk/swahili/kwa_kina/kenya_uchaguzi_2013.shtml

5.Na je vyombo vya habari?

Redio za lugha za asili, zilituhumiwa sana kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi. Mwandishi mmoja ni miongoni mwa wale walioshtakiwa kama washukiwa wakuu wa ghasia hizo. Baraza la waandishi wa habari nchini Kenya sasa limebuni sheria za utenda kazi kuwapa mwelekeo waandishi wa habari katika kazi yao.