Mjane aliyefukuzwa na mashemeji I.Coast

Mwanamke katika sehemu moja ya mashinani nchini Ivory Coast amealikwa kwenye mkutano nyumbani kwa chifu aweze kujitetea kwa nini aruhusiwe kurithi mali ya mumewe

Mama huyu hata hajafikisha hata miaka arobaini , kimya amekaa akitizama chini , chifu wa kijiji cha Guinkin, karibu na mpaka wa Liberia, ndiye anaongoza mkutano huu.

Mama huyu anaruhusiwa kuzungumza huku akijitambulisha: Naitwa Helene Tiro.''

"mume wangu alifariki miaka miwili iliyopita. Na sijui pa kwenda na watoto wangu,'' anasimulia huku akuoneakan kuzongwa na matatizo si haba.

"Natafuta ninavyoweza kudhibiti shamba langu ili niweze kuwalisha watoto wangu,'' anasema Helen. Ndugu za mume wangu wameuza shamba lote. Hata sijui pa kupata chakula kuwalisha wanangu.''

Kila mtu anamtizama Bi Tiro, wakiwa na mshangao nyusoni mwao, sio kwa sababu ya aliyoyasema bali kwa sababu amethubutu kuyatamka maneno hayo.

Sio jambo la kawaida kwa mama wa kijijini kuwa na ujasiri wa kuyatamka maneno kama haya dhidi ya familia zao.

"leo natafuta njia ya kuweza kupata shamba langu kutoka kwa watu hao ili niweze kujikimu kimaisha na kuwalisha wanangu,'' hatimaye Bi Tiro akasema huku akionekana kuwa na uchungu mwingi.

Anaongeza kuwa ana watoto saba na hana anavyoweza kutumia shamba lake ambalo amekuwa akilima tangu aolewe zaidi ya miaka ishirini iliyopita.

Mumewe ni mmoja wa maelfu ya watu waliofariki wakati wa ghasia za miezi sita ambazo zilizuka baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2010 wakati aliyekuwa rais Laurent Gbagbo, alipokataa kukubali kushindwa.

Bi Tiro hakumpoteza tu mumewe bali pia uwezo wake wa kujikimu kimaisha na wanawe.

<span >Mvutano wa sharia ya ndoa.

Kisa cha Bi tiro, sio nadra kutokea Ivory coast ambako utamaduni na mila hutumiwa kumpa mwanamke majukumu yake katika familia.

Mwezi Novemba mwaka jana, Rais Alassane Ouattara, aliyeingia mamlakani mwaka 2011, alivunja serikali kufutia mvutano kuhusu mabadiliko ya sharia ya ndoa, inayosema kuwa wanamue ndio wakuu wa nyumba na vhivyo wao ndio wasimamizi wa mali yote ya familia ikiwemo ardhi na mali nyinginezo. Katika maeneo ya vijijini, wanawake kawaida hawajui haki zao.

Baada ya Rais kuteua waziri mkuu mpya , mswaada ulipitishwa wa kuwafanya wanawake kusaidiana na waume zao kuwa wakuu wa nyumba.

Lakini sharia hiyo haijaweza kuleta mabadiliko yaliyotarajiwa katika nchi ambayo kwa karne imekuwa ikifuata mila zinazowapa wanaume uwezo zaidi kuliko wanawake kuhusiana na swala la uongozi manyumbani

"Leo sheria haijatofautisha kati ya wanaume na wanawake kuhusiana na swala la umiliki wa mali ya familia,'' anaelezea Maitre Kone Mahoua, makamu wa rais wa chama cha mawakili wanawake nchini humo.

"Lakini katika maeneo ya vijijini, imani na mila zenye athari kubwa bado zimekita mizizi, anaongeza Bi Mahoua.

Bi Mahoua anaelezea ambavyo wanawake wamedhalilishwa kwani wao ndio wanaolipwa mahari na ndiposa na wao machoni mwa wanaume ni kama mali yao.

Sio nadra katika baadhi ya jamii za kiafrika, wakati mume anapofariki, shemeji za bibi huona ni haki yao kumuoa au kumrithi mwanamke yule.

"tunapaswa kuanza kuhamasisha dada zetu walioko katika maeneo ya mashinani kuwa wana haki sawa na wanaume.

Wanawake kote duniani wanakabiliwa na changamoto za kunyimwa haki zao wakati inapokuja kwa swala la ardhi.

Wao huzalisha karibu nusu ya chakula kote duniani lakini baadhi ya nchi wanamiliki asilimia mbili tu ya ardhi kulingana na takwimu za umoja wa mataifa.

Huku viongozi wa dunia wakijiandaa kwa mkutano wa nchi nane zilizostawi duniani, G8, maswala kuhusiana na umiliki wa ardhi yanatarajiwa kupewa kipaombele kwenye ajenda ya mkutano huo.

Umoja wa mataifa na mashirika ya kimataifa wanayadai kuwa ikiwa wanawake watapewa haki za umiliki wa ardhi na mali nyinginezo , wataweza kuzalisha chakula zaidi na hivyo kupunguza njaa duniani.

Mizozo ya mashamba

Pamoja na tamaduni zilizokita mizizi, wanawake nchini Ivory Coast, wamekabilia na changamoto nyingine kuhusiana na umiliki wa ardhi.

Kwa zaidi nya mwongo mmoja uliopita ya misukosuko, raia wa Ivory Coast, ametoroka mashamba yao, na wakati wa mizozo kama hiyo wanawake kunyanyaswa kuhusiana na hakli zao za umiliki wa mali.

Maelfu wametoroka makwao katika miaka kumi iliyopita kutokana na mizozo, na walipokuwa wanatoroka, ardhi waliyoacha ikiwa na rotuba, ilitwaliwa.

Wanawake kama Bi Tiro, wamepoteza waume zao , watoto wao , ndugu na dada zao, nyumba zao na mashamba yao.

"swala la ardhi limekuwa tatizo kubwa kwa muda mrefu, lakini kulingana na mzozo uliopita, hali imezidi kuwa mbaya zaidi," anasema Batio Etienne, chifu wa mji wa Guinkin.

Na wakimbizi anapoendelea kurejea nyumbani ndipo swala la ardhi linaendelea kuwa tatizo sugu kwani mivutano nayo inaendelea kukithiri.

Chifu Etienne anasema kuwa watu wako tayari kupigania ardhi ambayo imekuwa ikimilikiwa na familia zao kwa miaka mingi, liwe liwalo.

Mkutano huu wa kujadili hali ya Bi Tiro sio wa kwanza wa aina yake.

Chifu anasema kuwa huenda Bi Tirro akachangia shamba hili na mtu aliyelinunua kuwa kwa familia ya mumewe.

Sio jambo zuru lakini hakuna anayetaka kuona damu ikimwagika kwa sababu ya shamba.

"Ikiwa familia ya mume wangu haitaki, mimi nitafanyaje?"anahoji bi Tiro.

"Siwezi kutumia nguvu . Hakuna ninachoweza kufanya kama mwanamke."