Wanawake waliopinga utamaduni na kushinda

Katika nchi nyingi za Afrika wanawake wamekuwa wakibaguliwa katika urithi wa mali ya familia kwa sababu tu ya wao kuwa ; wanawake hiyo ikiwa na matokeo ya kuizingatia mila na desturi zinazolenga kumnyanyasa mwanamke.

Hivi karibuni imekuwa tofauti kwa wanawake wanne nchini Bostswana waliojikuta huzuni yao ikigeuka furaha baada ya uamauzi wa mahakama ya rufaa nchini humo kuamua kurejesha ardhi kwa wanafamilia hao wa kike waliotaka kupoteza haki yao urithi wa familia kwa sababu tu wao kuwa wanawake kwa misingi ya mila za jamii yao.

Mwezi uliopita uamuzi wa mahakama rufaa ulileta furaha kwa wana famialia Edith Mmusi (80),na wadogo zake Bakhani Moima,Jane Lekoko,na Mercy Ntsehkisang ambapo katika kijiji chao cha Kanye kusini mwa mji wa Gabarone Bi.

Mmusi anaelezea hadithi ndefu ya kesi yao kuhusiana na umiliki wa ardhi ya familia

Akiwa katika eneo lake kijijini kwao Kanye Mmusi akionekana mwenye uso wa furaha na tabasamu alielezea kilichomkumba yeye na wanafamilia wenzake wanawake hadi kutaka kubaguliwa kurithi sehemu ya mali ya familia hadi uamuzi wa mahakama ulipowasaidia

“Ilinibidi kuwa na ujasiri katika muda mrefu wa kufuatilia suala hili na ilikuwa ni huzuni kwa familia na kwa siku nyingi nilikuwa sipati hata usingizi nikiwaza utatuzi wa jambo hili lakini mwishoni limefanikiwa nina furaha isiyo kifani”alisema Mmusi

Mmus akionyesha mabaki ya nyumba iliyokuwa nyumba yao wakati wa wakiishi na wazazi wao waliofariki alisema kuwa kulikuwa na nyumba nane katika eneo lao kwaajili ya kumudu familia yao na kwamba wao pia walichangia katika ujenzi wa nyumba hizo na ukarabati wake hivyo ni sehemu ya warithi halali

Mara baada ya baba yao mzazi kufariki Mmusi na wadogo zake wa kike walikuwa wakifanyia marekebisho ya majengo hayo huku wakiwa wanaishi na mama yao mzazi aliyefariki baadaye mwaka 1988 na kwamba wao walikuwa pia sehemu ya familia na ukizingatia kwamba walitumia sehemu ya fedha zao kuliendeleza eneo hilo

Wakipinga kunyimwa haki ya kurithi eneo hilo la familia katika utetezi wake mahakamani Mmusi alisema wao ni sehemu ya eneo hilo la familia na kwamba wanastahili kurithi eneo hilo japo kuwa kwa misingi ya mila na desturi za Botswana nyumba ya familia inapaswa kurithiwa na motto wa kwanza wa kiume ama mtoto wa kiume wa mwisho.

Kwa mjibu wa mila za Botswana ilipitishwa kwamba Mmusi na wenzake waliamriwa na mahakama hiyo kuondoka katika nyumba kama sehemu ya kuheshimu taratibu na mila za jamii hiyo,hata hivyo baadhi ya ndugu wa kiume waliona hatua ya wanawake hao kudai sehemu ya urithi ni sawa na kudhalilisha familia nzima na jamii inawaona kama wasaliti wa mila

Hata hivyo ili kupinga maamuzi ya mahakama hii ya kijadi Mmusi na wenzake walikata rufaa mahakama kuu na kisha kupewa haki ya kurithi eneo hilo kinyume na sheria na taratibu za mila na hivyo kurejeshewa furaha yao.

Pamoja na uamuzi huo ambao umewapa haki Mmusi na ndugu zake lakini anasema kwa sasa ndugu zao hasa wakiume wamekuwa wakiwaona kama wasaliti wa mila na desturi na hivyo kuwanyooshea vidole jambo ambalo anaamin litafikia mwisho wake hasa katika ulimwengu huu wa mfumo mpya wa maisha

Baadhi ya wanaume wanahisinkuwa wanawake wanahujumu tamaduni zao kwa kuzipinga

Wanawake wengi wanatumai kuwa dhana hii itakuja kubadilika muda unapokwenda.