Uingereza kukuza masoko ya kiisilamu

Kongamano la kiislamu kuhusu maswala ya fedha linafanyika mjini London.

Waziri mkuu David Cameron amechukua nafasi hiyo kutangaza maazimio yake ya kuimarisha hali ya biashara katika mji wa London wakati huu ambao biashara inakua kwa kiwango kikubwa.

Serikali ya Uingereza imekuwa makini kuistawisha London ili mji huo uvutie shughuli za kibiashara.

Hii inalingana na juhudi za waziri wa fedha George Osborne kufanya mji huo kuwa uwanja wa biashara kutumia sarafu ya uchina Renminbi.

Cameron anasema kuwa hazina ya fedha ya Uingereza imeanza kushughulikia dhamana zinazotumika kwa masharti ya kiisilamu ili kuchangisha dola milioni miambili, na ambayo itazinduliwa mwaka ujao.

Uuzaji wa dhama za serikali ndio njia ambayo serkali nyingi hutumia kukopa pesa kutoka katika masoko ya kimataifa.

Mjadala wa wasomi

Njia maalum inayotambulisha huduma za kifedha zinazofuata sheria za kiislamu ni inayozingatia kutokuwepo kwa kulipa ama kuchukua riba ,huwa zinachukuliwa kama uwekezaji tu wala si kama mkopo.

Kwa kawaida malipo ya kwanza hufanywa kwa njia ya uwekezaji katika biashara Fulani badala ya mkopo kama kwa vile mwekezaji muislamu katika serikali ya uingereza kIsha malipo kwa mwekezaji ni kwa njia ya kodi ama faida badala ya riba

Uhusiano wa kifedha utakao fanywa na serikali ya Uingereza utatumia mali kama majengo na ardhi kama njia ya uwekezaji

Mwelekeo huu umepata upinzani kutoka kwa wataalamu wa maswala ya kiislamu wakisema kuwa hautazuia ulipaji wa riba kwa sababu ada za uwekezaji zinatoshana na zile za riba

Hata hivyo kuna mjadala mkubwa kati ya wasomi wa kiislamu kuhusu vitendo vinavyo kubablika na visivyo kubalika na pia serikali ya Uingereza haijakamilisha mipango kadhaa ya serikali katika maeneo ya nchi za kiislamu hawatumii njia hii ili kuchangisha pesa ikiwemo Indonesia,Malaysia na Uturuki wameanza kuchukua mwelekeo huo.

Bwana Cameron amesema kuwa Uingereza itakua nchi ya kwanza kando na nchi za kiislamu kuanza kutumia mfumo huo wa kifedha.

Aliongeza kuwa soko la hisa la London itaanzisha rasmi kuorodhesha hisa za biashara zinazotumia mfumo wa kifedha unaofuata sheria za kislamu Kitendo hiki kurahisha uamuzi wa waekezaji wa kiislamu wa kuchagua mahali pa kuweka fedha zao

Nafasi za biashara

Uwekezaji wa kiislamu ni biashara inayonoga sana na Waziri mkuu amesema kuwa kwa sasa biashara hii inakuwa kwa asilimia 50% zaidi kuliko benki za kawaida.

Kukopa kunakokotoza riba bado ndio njia inayotumika na serikali za kiislalu zinazohitaji fedha kutoka masoko au mashirika kama IMF na benki ya dunia na nyingi bado zina uwekezaji ulio na riba kama vile serikali ya Marekani

Hata hivyo mashirika ya uwekezaji wa kiislamu duniani yanatabiri kufikia dola trilioni 2 kufikia mwaka ujao kulingana na hesabu za EY