Ujumbe wa Mhariri

Ujumbe wa Mhariri

Shukran sana mpenzi wa Sema Kenya kwa kuandamana nasi katika safari ya msimu wa pili wa Sema Kenya iliyoanza mwezi Juni mwaka jana.

Katika msimu huo wa pili tulipata fursa ya kuzuru sehemu mbali mbali nchini Kenya. Na katika safari hizo tuliwapa nafasi wananchi kukutana ana kwa ana na viongozi wao na kuwahoji kuhusu maswala yanayohusu ugatuzi na utenda kazi wa serikali hizo ndogo 47 nchini Kenya.

Katika kipindi hicho cha karibu mwaka mmoja pia tulipata ya kuandaa kipindi maalum cha kusherehekea miaka 50 tangu Kenya ijipatie uhuru wake.

Na mara tu palipotokea shambulizi ya kigaidi katika maduka ya kifahari ya Westgate Mall, Sema Kenya ilitafuta majibu kutoka kwa viongozi kwa kuwakutanisha viongozi, wachanganuzi wa maswala ya kiusalama, walioathirika na shambulizi hilo a halikadhalika wananchi wa kawaida.

Hivyo tarehe 2 Februari, 2014 tunahimisha msimu wa pili wa Sema Kenya.

Hata hivyo kuanzia Jumapili tarehe 9 Februari, 2014, tegea Idhaa ya Kiswahili ya BBC muda ule ule wetu wa kawaida, saa saba mchana saa za Afrika Mashariki ufurahie vipindi maalum vya marejea vilivyo "pikwa upya". Bila shaka, utafrahia.

Haki miliki ya picha BBC MA
Image caption Katika maandalizi ya mjadala

Lakini usiende mbali, Sema Kenya imerudi jikoni kukuandalia Msimu wa Tatu, sehemu hii tutajikita zaidi katika kuwawajibisha zaidi viongozi, kuwapiga darubini na kuangalia maswala ya utawala, utoaji wa huduma na matumizi ya m

pesa za umma. Itakuwa ni fursa nyingine ya kukukutanisha wewe na viongozi wako ili upate majibu ya maswali yako.

Msimu wa tatu utakuwa moto zaidi na bora zaidi.

Image caption Odhiambo Joseph