Mjadala wa Murang'a kwa Picha

19 Januari 2014 Imebadilishwa mwisho saa 08:26 GMT

Mjadala huu uliangazia jinsi kaunti hii inapanga kuzalisha pesa za matumizi ya kaunti.
Murang'a ni mojawapo ya kaunti tajiri nchini ikiwa na ardhi bora ya ukulima.
Kaunti hii imeanzisha mradi wa Shilingi kwa Shilingi ili kuzalisha pesa za matumizi ya kaunti ikitumia uwekezaji wa wenyeji.
Sema Kenya ilizuru Murang'a kuwapa wananchi nafasi ya kujadili mradi huu pamoja na viongozi wao.
Viongozi walijitokeza kujibu na kukariri masuala ya uwekezaji katika kaunti.
Wananchi walipata nafasi bora ya kuuliza maswali.
Ni njia ipi bora ambayo kaunti zinaweza kutumia kuzalisha pesa za kuendesha miradi tofauti?
Mjadala ulichangamsha na kuelimisha viongozi na wakazi wa Murang'a.