Shabiki wa Sema Kenya

Shabiki wa Sema Kenya

Image caption Mariah Hose

Wiki hii shabiki wetu ni Mariah Hose ambaye amefuata msimu wa pili wa Sema Kenya kwa makini sana na kujadili maswala katika ukurasa wetu wa kijamii wa Facebook - BBC Sema Kenya.

Msimu huu mijadala mengi imegusia migogoro kwenye uongozi wa kaunti, na Mariah alikuwa na haya ya kusema kuhusu tatizo hili:

"Matatizo ya uongozi yapo kila pahali. Hawa magavana ni shida kuu kwa uongozi kwa sababu wanataka kufanya kazi kivyao, wanajiona wakiwa na mamlaka sana, poleni watu wa Kwale hata kwetu (Laikipia) shida ni zile zile." Mariah Hose.