Gravity na 12 years a slave zatamba

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alama zinazowakilisha tuzo za Bafta

Sinema ya Gravity iliyoongozwa na Alfonso Cuaron ilijinyakulia tuzo sita, huku sinema ya 12 years a slave imetangazwa kuwa filamu bora, katika tuzo za Bafta zilizofanyika siku ya jumapili jijini London.

Sinema ya the space drama ilitangazwa kuwa sinema bora ya uingereza na kujinyakulia zawadi nyingine kwa ajili ya ubora wa picha, Sanaa ya upigaji picha,sauti bora na sauti yenye uhalisia, huku Alfonso Cuaron akijinyakulia tuzo ya mwongozaji bora wa sinema.

Nyota wa uingereza Chiwetel Ejiofor alipata tuzo ya Bafta ya muigizaji bora akicheza kwa jina la Solomon Northup katika sinema ya 12 Years a Slave, huku Cate Blanchett akitangazwa muigizaji bora katika sinema ya Blue Jasmine.

Mwongoza filamu wa Uingereza,Steve McQueen alipata tuzo ya filamu bora ambayo 12 Years a Slave ilipata ushindi

Ejiofor a,baye aliteuliwa katika kinyang’anyiro cha tuzo za Bafta miaka saba iliyopita kama nyota anayechipukia, alipokea tuzo hiyo kutoka kwa Muigizaji wa filamu Uma Thurman.

Filamu ya Great Gatsby ilishinda tuzo mbili, ya utengenezaji mzuri wa filamu na ubunifu wa mavazi.

Room 8 ilijinyakulia tuzo ya filamu fupi bora na zawadi ya filamu fupi bora ya vikaragosi ilinyakuliwa na filamu iitwayo Sleeping with the Fishes.

Tuzo ya filamu bora ya vikaragosi ilikwenda kwa waandaaji wa filamu iitwayo Frozen ambayo ilizishinda zile za Monsters University na Despicable Me toleo la pili.

Bafta ni tuzo kubwa zaidi kutolewa kwa sekta ya filamu duniani kabla ya tuzo za Oscars tarehe 2 mwezi Machi.