Mtayarishi "Mambo ni moto sana!"

Tunaendelea kukuletea Mjiadala mtoto moto

Image caption John Ohaga (kushoto), akiwakaribisha waliohudhuria mjadala wa kwanza wa msimu huu.

Shabiki wetu mheshimiwa, baada ya mapumziko mafupi, kipindi ukipendacho cha majadiliano cha Sema Kenya sasa kimerudi.

Tamaduni zetu za BBC zinatilia maanani utayarishaji wa vipindi vya hali ya juu. Hivyo basi, msimu huu unaandaliwa kwa ufanisi tukimulika masuala sugu katika jamii. Tunalenga watazamaji wa tabaka mbali mbali, kutumia mbinu tofauti tukiwa watangazaji wa kisasa.

Tunao wana jopo ambao ni wataalam katika sekta tofauti na washiriki wengi kwenye studio. Mbali na hawa, baadhi ya watarihi wetu wanazunguka sehemu tofauti, pamoja sehemu zilizotengwa nchini wakiandaa mijadala midogo ambayo inaunganishwa na mjadala wa studio. Muundo huu mpya unahakikisha kwamba sauti za wanyonge na waliotengwa, zote zinasikika. Kwa kweli msimu huu wa tatu utafana sana.

Utafiti unaashiria kwamba vipindi vinavyolenga usahii wa masuala, vinashawishi utawala bora katika jamii na pia katika mazingira tofauti. Sema Kenya ni mojawapo wa vipindi kama hivi, na kinawapa wananchi jukwaa la kushiriki katika mazungumzo yanayolenga sera mbadala.

Shabiki mpendwa, tunakualika kushirki katika mijadala kwenye kurasa zetu za kijamii za Twitter na Facebook. Vipindi vyote pia vinapatikana katika mtandao wetu BBC Sema Kenya.

Kipindi kitapeperushwa hewani kupitia KBC Channel 1 kila Jumapili saa kumi na mbili jioni, na kurudiwa kila Jumatano saa nne usiku. BBC Swahili, KBC Idhaa ya taifa na redio washirika kumi na wanne pia watakipeperusha kipindi. Hivi, sio rahisi kwamba utapitwa na kipindi!

Sema Kenya ni nafasi yako ya kujiunga na mazungumzo ya kitaifa ukiwa unaijenga nchi ya Kenya kama unaivyoipenda.