Huwezi kusikiliza tena

Je viongozi wa kenya wanaheshimu sheria?

Tunaangazia swala la demokrasia na utawala bora. Juhudi nyingi zeimefnywa na wengi kuleta madadiliko ya kijamii na kuhimiza uongozi wa kuzingatia sharia.

Lakini licha ya yote hayo, mabadiliko ya kijamii yako wapi? Tumeyafikia kweli? Utawala bora unaozingatia sheria tunauona kweli?

Image caption Kwanza kabisa ni Dkt Willy Mutunga , Jaji mkuu wa Kenya na Kamshina Catherine Mumma, kamati ya utekelezaji katiba

Kupambana na swala hili tuna wageni wawili mashuhuri katika jopo letu hapa studio.

1) Kwanza kabisa ni Dkt Willy Mutunga – ambaye ni Jaji Mkuu wa Kenya na pia Rais wa Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya. Kwa miaka mingi alikuwa mtetezi mkali wa haki na demokrasia.

2) Mgeni wetu wa pili ni Bi Catherine Muyeka Mumma – Yeye ni Naibu Mwenyekiti wa tume ya taifa inasimamia utekelzaji wa katiba. Pia ni mwanasheria na mtalaam wa maswala ya haki za binadamu.