Huwezi kusikiliza tena

Tatizo la ardhi Kenya in bomu?

Wakati Kenya ilipokuwa ikipigania uhuru, ajenda mbili kuu zilikuwa ni uhuru na ukombozi wa mashamba. Uhuru ulipatikana;lakini je, mashamba yetu yako huru?

Licha ya juhudi za serikali nne nchini Kenya kutatua swala nyeti la ardhi , mambo yamezidi kunyeta zaidi huku baadhi ya wakenya wakishuhudia dhuluma katika ardhi zao.

Kenya ilipopata katiba mpya mwaka 2010, matumaini yalikuwa sufufu kuwa angalau vuta nikuvute la ardhi lingesuluhishwa au hata kupunguzwa hususan kufuatia kuundwa kwa tume ya kitaifa ya ardhi.

Lakini je, ndoto hiyo itatimia?

Wanajopo wetu ni pamoja na:

1. Abigail Mbagaya Mukolwe- Naibu mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi. Pia ana tajiriba kubwa katika maswala ya usorovea na vita dhidi ya ufisadi.

2.Mheshimiwa Abdullahi Jaldesa Banticha-Mbunge wa Isiolo Kusini

3.Mheshimiwa Shakila Abdalla Mohamed –Muwakilishi wa wanawake wa Lamu, Bungeni na ni anaketi kwenye kamati ya bunge la taifa kuhusu ardhi.

4. Odenda Lumumba- Mtaalam wa maswala ya ardhi na mshirikishi wa kitaifa wa Kenya land alliance.

5. Pamoja na Mheshimiwa Richard Kalembe Ndile-Aliyekuwa mbunge na pia waziri msaidizi. Yeye hujiita mtetezi wa maskwota.

Washiriki ni kutoka maeneo ya Lamu, Taita Taveta, Kibwezi, Eldoret na Mount Elgon.

Shiriki katika majadala wa BBC Sema Kenya kwa kutuma neno SEMA kwa nambari 22340. Huduma hii haitozwi malipo