Huwezi kusikiliza tena

Ufisadi unaweza kumalizika Kenya?

Licha ya kamati na tume mbali mbali kuwahi kubuniwa nchini Kenya kama njia moja wapo ya kupambana na ufisadi lakini tatizo hilo sasa linaonekana kuwa ndio hali ya kawaida ya maisha ya wakenya.

Hii ni kusema ufisadi umeshika mizizi katika maisha ya wakenya kiasi cha kwamba hauwezi kumalizika?

Na je serikali, viongozi na wananchi wa kawaida kweli wana ari na zma ya kupambana na ufisadi?

Hii ndio mada ya mjadala huu?

Image caption Mumo Matemu

Jopo la kujadili mjadala huu ni:

1 Bwana Mumo Matemu- Mwenyekiti wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi

2. Bi Sophia Lepuchirit- mwanachama wa kamati ya kitaifa ya kuendesha kampeni dhidi ya ufisadi

3. Bwana Samwel Kimeu- Mkuu wa shirika la kushirika la kupambana na ufisadi-Transparency International, tawi la Kenya.

Washiriki ni wananchi kutoka sehemu mbali mbali nchini Kenya