Libya kupambana na wanamgambo

Image caption Mji wa Tripol

Serikali ya Libya imesema imeamuru vikosi vyake kuingia mjini Tripoli kupambana na wanamgambo wenye silaha katika mapigano yaliyodumu kwa mwezi mmoja nchini humo.

Muungano wa makundi hayo ulifanikiwa kuwaondoa mahasimu wao waliokuwa wakiunga mkono Serikali, kisha wakaunda serikali ya pamoja.

Serikali ya Libya imesema imeamuru vikosi vyake kuukomboa mji wa Tripoli na taasisi za serikali ya nchi hiyo kutoka mikononi mwa watu wanaodaiwa kuwa na silaha ambao walifanya mashambulizi ya mabomu mjini Tripoli mwezi Agosti mwaka huu.

Jeshi la nchi hiyo linahusisha pia wanamgambo wanaoiunga mkono Serikali, lakini hakuna vikosi vyovyote vilivyo karibu na mji huo tangu wakati wa majira ya joto.

Wito umetolewa kwa wakazi wa mjini Tripoli kuunga mkono mpango wa serikali halikadhalika kufanya mgomo mjini humo dhidi ya wanaotawala eneo hilo.

Serikali iliyochaguliwa ina makao yake mashariki mwa Libya lakini serikali pinzani iliweka makazi yake mjini Tripoli mwezi Septemba.