Mume ajilipiza kisasi kwa kuua mamba

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Batambuze na silaha iliyompa ushujaa.

Yapata miezi minne sasa mwanamke mmoja aitwaye Demeteriya Nabire alipouawa na mamba wakati alipokwenda ziwani kwa ajili ya kwenda kuteka maji . Na ndipo akumbana na mamba huyo na kumla.lakini baadaye Mamba huyo alirejea na kumkuta mume wa Nabire akimsubiri tayari kwa kujilipiza kisasi.

Demeteriya Nabire alikuwa ukingoni mwa ziwa na wanawake wenziwe wanao toka kijiji kimoja wakichota maji kutoka katika ziwa linalotokea nchini Uganda ziwa Kyoga na mara mamba akamdaka.alimkokotea mbali ziwani na hakuonekana tena.

Mume wa mwanamke huyo ,Mubarak Batambuze, alichanganyikiwa kwani mkewe alikuwa mja mzito pindi alipokutwa na umauti,na amepoteza watu wawili si mmoja akiwemo mtoto aliyekuwa tumboni.Mubarak aliishiwa nguvu.lakini mwezi uliopita alipata taarifa kuwa mamba yule yule aliye mletea maafa amerejea tena.

Mubarak anasema kwamba ,alikuja mtu akaniita akisema Mubarak nina taarifa kwa ajili yako,yule mamba aliyemla mkeo yuko hapa kijijini,na sisi tunamtafuta.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 50 ambaye shughuli yake kubwa maishani ni uvuvi,aliinuka na kuelekea ziwani akifuatiwa na rafikize anaeleza jinsi walivyoanza kupambana na dubwana hilo kubwa ,walijaribu kupambana nalo kwa mawe na fimbo,lakini hawakufanikiwa na mara Batambuze akaamua kwenda kwa muhunzi mmoja kijijini hapo.

Anasema alipofika kwa muhunzi alimweleza alikuwa akipambana na mnyama aliyemla mke na mtoto aliyetumboni,na sasa nataka kujilipiza kisasi nahitaji zana madhubuti hasa ,na akamtaka mhunzi amtengenezee mkuki madhubuti ambao utamwezesha kumuua mamba huyo.

Mhunzi akataka ujira wa paundi 3.20 sawa na dola 5 na tukafikia makubaliano akanitengenezea mkuki huo, ilikuwa ni gharama kwangu Batambuze ,lakini kwa ajili ya mke na mwanangu niliitoa pesa hiyo.

Batambuze akautwaa mkuki wake na kuelekea ziwani,mkuki ulitengenezwa upande mmoja ukiwa na kitu kama ndoano, na mgane huyo akaelekea kwenye mapambano.

Alipofika ziwani mamba alikuwepo kama aliyekuwa akimsubiri hivi,na marafiki zake Batambuze wakaanza kumtisha,wakimtaka asipambane na dubwana hilo,ni kubwa mnooo,litamtafuna na yeye pia,mkuki wako alionao si lolote mbele ya dubwana hilo,hautamsaidia kitu,

Lakini Batambuze akawataka wao wabaki ,yeye atakabiliana nalo,akiwaambia hatajali akiliwa na yeye pia nitamuua kwa mkuki huu,na nitahakikisha anakufa.

Mamlaka ya wanyama pori nchini Uganda imemuelezea mamba huyo kuwa ana zaidi ya mita nne na uzito wa kilo mia sita anasema Oswald Tumanya.

Batambuze akaufunga mkuki Kamba mwishoni ili akiutupia na kumchoma mamba huyo iwe rahisi kumvutia nje ya maji kumpunguza nguvu na kumshambulia, maana nguvu ya mamba iko kwenye maji,haikuwa kazi rahisi tulipambana mno na hofu ikaniingia.

Watu nao wakapata hofu waka anza kurejea kijijini,ilikuwa ni tafrani kubwa,lakini baadaye nilipofanikiwa kumuua mamba huyo wakaja kumtazama na wakashangazwa na ukubwa wa mamba huyo,si mamba wa kawaida na watu wakaniita mimi shujaa. Anasema Batambuze .

Image caption Mamba aliyeuawa,mwenye ukubwa usio wa kawaida

Mamba huyo akachukuliwa na chuo kikuu cha Makerere kilichoko mjini Kampala kwa uchunguzi zaidi,na mchunguzi aliyekabidhiwa kazi hiyo ni Wilfred Emneku, ambaye baadaye baadaye alisema kwamba aligundua mfuba wa binaadamu tumboni mwa mamba huyo ingawa bado anafanya utafiti zaidi.

Mtaalamu wa mamba kutoka katika chuo kikuu cha Charles Darwin University nchini Australia, Adam Britton, amesema kwamba hashangazwi na mifupa ilikutwa tumboni mwa mamba huyo kuwa ni ya Demeteriya Nabire.Baada ya wiki kumi na mbili,katika hali ya kawaida ,si jambo la kawaida kukuta mabaki yam lo uliopita kusalia tumboni mwa mamba .

Wakati Batambuze akisherehekea ushujaa wake kijijini,hatakuwa na kaburi la kuomboleza kifo cha mkewe,amebaki na sifa za wanakijiji wenziwe waliokuwa na hofu ya kuliwa na mamba huyo lakini wako huru sasa kwenda kuteka maji bila hofu yoyote.