Mji wa dhahabu unaongoza kwa mabilionea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mji wa Jonannesburg

Mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini ndio mji ulio na idadi kubwa zaidi ya watu tajiri barani Afrika.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na benki ya AfrAsia na jarida la New World Wealth.

Mji huo unaofahamika kwa mji wa dhahabu, ina watu wapatao 23,400 ambao ni mamilionea.

Inakisiwa kuwa asilimia 30 ya mamilionea barani Afrika wanaishi Afrika Kusini.

Misri ni ya pili ikiwa na mamilionea 10,200, Nigeria ni ya tatu ikiwa na 9,1000.

Haki miliki ya picha SAFODIENAFP
Image caption Maeneo ya kifahari mjini Johannesburg

Utafiti huo umechukua takwamu ya watu ambao wana zaidi ya dola milioni moja pekee.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa barani afrika kuna mamilionea 163,000 ambao kwa pamoja mali yao yote inakisiwa kuna dola bilioni 670.

Inashangaza kuwa mji wa Johannesburg, ina idadi kubwa na mamilionea kuliko Lagos, mji ambao unakisiwa kuwa mji mkubwa wa biashara barani Afrika, kwa sababu Nigeria pia ina idadi kubwa zaidi ya watu na uchumi wake ndio mkubwa zaidi barani.

Image caption Barabara mjini Lagos

Hata hivyo uchumi wa Nigeria ulianza kukua hivi karibuni lakini Afrika Kusini imekuwa kileleni kwa miaka nyingi.

Mtaalamu wa masuala ya uchumi, Owen Nkomo na mwanzilishi wa kampuni ya uwekezaji ya Inkunzi, amesema kuwa fedha kutoka kwa mauzo ya hisa za kampuni za Wazungu katika soko la hisa la Johannesburg, zilitumika vyema, licha ya kuwa kampuni nyingi bado zinamilikiwa na raia wa nchi hiyo walio Wazungu.

Amesema mpango wa serikali ya kuwapa Waafrika uwezo zaidi kiuchumi, ili kupunguza pengo kati ya Wazungu na Waafrika ni sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi ya Waafrika walio mamilionea.

Licha ya utajiri huu wote, Afrika Kusini bado ingali inakabiliwa a tatizo kubwa ya ukosefu wa ajira na umasikini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maeneo ya kifahri ya Sharm el-Sheikh nchini Misri