Wanawake nchini Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake waoa wake wenzao Tanzania

Katika mila, desturi na utamaduni wa makabila mengi muundo wa familia hasa ndoa hutofautiana, wakati nyingi zikiwa zikisihirikisha mwanaume na mwanamke, katika mkoa wa Mara, wilaya ya Tarime, kaskazini mwa Tanzania, utamaduni wa enzi unahusisha wanawake kuwaoa wanawake wenzao. Mwandishi wa BBC ,Tulanana Bohea anatuarifu zaidi namna muundo wa familia mbadala wa Nyumba ntobhu umebadilika na kuwa wa kisasa zaidi.