Soka yatumiwa kubadili vijana gerezani

Image caption Wafuasi wa Boko Haram waliokamatwa wakicheza mpira katika gereza moja nchini Nigeria

Wapiganaji wa Kiislamu nchini Nigeria, wanaotumikia vifungo vyao jela, sasa wameamua kucheza kandanda kama mpango wa serikali wa kuwapa mafunzo ya kuachana na misimamo mikali ya Kiislamu.

Wafungwa hao walio katika magereza kadhaa nchini humo hutumia muda mwingi kufanya mazoezi.

Maafisa wa idara ya mahakama mara kwa mara huanda mashindano miongoni mwa timu mbali mbali za wafungwa.

Kila asubuhi wafungwa hao kupelekwa uwanjani kwa mafunzo ya mchezo huo.

Wapiganaji wa Kiislamu nchini humo wamepiga marufuku michezo ya aina yoyote na wafungwa hao walio na umri wa kati ya miaka 20-30 kukubali kucheza ni ishara nzuri kuwa wameanza kuacha mienendo yao ya zamani.

Mbali na michezo wafungwa hawa pia hupewa mafunzo ya kidini.

Image caption Miongoni mwa wafungwa hao kuna wale ambao ni wachezaji wazuri wa soka

Wakati wanapocheza katika uwanja wao ndani ya jela, mafunzo ya dini ya Kikristu huwa inaendelea katika kanisa moja iliyoko karibu na uwanja huo, kwa dhamira ya kuwafunza wafungwa hao jinsi ya kutengamana na makundi mengine.

Mfungwa mmoja aliiambia BBC kuwa wakati walipofikishwa katika jela hilo, hakuwa akiitikia maagizo yoyote kwa wa walinzi wa gereza hilo.

Anasema mara nyingi walikuwa wakizozana na hakuwachukulia kama binadam, lakini sasa asema mambo yamebadilika.