Mazoezi kusaidia saratani ya tezi dume

Haki miliki ya picha
Image caption Celi za zinazosababisha saratani

Watafiti nchini Uingereza wameanza kufanya majaribio ikiwa mazoezi ya mwili yanaweza kuwasaidia wanaume wanaoungua saratani ya tezi dume.

Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield Hallam wanashirikiana na taasisi ya utafiti wa matibabu ya saratani ya Uingereza.

Wanasema watafiti hawa kwamba wana imani mazoezi ya mwili yanaweza kuzuia saratani hiyo kusambaa maeneo mengine.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Saratani ya tezi dume

Watafiti hao wamewaomba wanaume ambao wana saratani ya tezi dume ambayo haijasambaa kujiunga na majaribio haya kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mazoezi ya viungo hutumiwa kama matibabu, na wanaume kadhaa watafanyiwa mazoezi hayo kila wiki. Wengine watashauriwa jinsi ya kufanya mazoezi kama hatua ya kusaidia matibabu ya saratani ya tezi dume.

Ikiwa mazoezi hayo yasaidia kupunguza kusambaa kwa saratani hiyo wanasayansi wanasema yataambatana na matibabu ya saratani ya tezi dume.